BIA, SIGARA VINYWAJI VIKALI KUPANDA BEI


Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William MgimwaSerikali imeoongeza kodi kwenye magari makuukuu, bia,  vinywaji vikali, na baridi ambavyo kodi imekuwa ikiongezwa kila mwaka na kuwathiri watumiaji.

Kutokana na hali hiyo wanywaji pombe na sigara watalazimika kutumia fedha nyingi ili kupata huduma hizo.

Bidhaa zisizokuwa za mafuta ambazo zimefanyiwa marekebisho na kuongezwa kodi ni mvinyo, pombe, vinywaji vikali, na sigara. Vinywaji hivyo vimeongezwa kodi kwa asilimia 10.

Kutokana na bajeti ya mwaka 2013/14 iliyosomwa jana bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa, Vinywaji vikali vimepanda kutoka Sh2,392 hadi Sh2,631 kwa lita  sawa na ongezeko la Sh239 kwa lita moja.

Bia inayotengenezwa kwa nafaka nchini ambayo haijaoteshwa imeongezwa kodi kutoka Sh310 kwa lita hadi Sh341 kwa lita, sawa na ongezeko la Sh31 kwa lita.

Pia bia nyingine zote zimepanda kutoka Sh525 kwa lita hadi Sh578 kwa lita sawa na ongezeko la Sh51 kwa lita.

Kwa upande wa vinywaji baridi, vimepanda kutoka Sh83 kwa lita hadi Sh91 kwa lita sawa na Sh na ongezeko la Sh8 kwa lita.

Vile vile sigara zenye kichungi na zinazozalishwa nchini zimepanda kwa asilimia 75, kutoka Sh19,410 hadi Sh21, 351 kwa sigara 1,000 sawa na ongezeko la Sh1.94 na senti 94 kwa sigara moja.

Ushuru pia umeongezwa kwenye magari yasiokuwa ya uzalishaji na yenye umri wa miaka 10 kutoka asilimia 20 mpaka hadi asilimia 25.

Dk Mgimwa alisema hatua hiyo imelenga kupunguza uagizaji wa magari  chakavu  ili kulinda mazingira na kupunguza ajali za mara kwa mara.

Uamuzi wa serikali kuongeza kodi katika maeneo hayo na mengine, utaisaidia serikali kuongeza mapato ya Sh510 bilioni.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo