WATU BINAFSI MAKETE WAKONGA NYOYO ZA WAFANYAKAZI WAO KWA ZAWADI MEI MOSI

Diwani wa viti maalum tarafa ya Lupalilo wilayani Makete Bi Kazindogo, akifafanua zawadi alizotoa yeye binafsi tsh 20,000/= kwa wenyeviti wote wa vijiji vya kata ya Iwawa, mfanyakazi binafsi wa vinywaji kwenye depo ya Livungu, pamoja na chakula cha mchana kwa watendaji wote wa vijiji kata ya Iwawa, hapa akifafanua kuhusu zawadi hizo
Mwenyekiti wa mojawapo ya vijiji vya kata ya Iwawa wilayani Makete akipokea zawadi yake kutoka kwa mgeni rasmi katika sherehe ya mei mosi Makete
Mkurugenzi wa shirika la SUMASESU wilaya ya Makete, Egnatio Mtawa akifafanua kuhusu zawadi ya Mei mosi kwa wafanyakazi wake, ambapo alisema kwake wafanyakazi wote ni bora, hivyo amewazawadia kwenda Matema Beach kwa siku tatu, mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu
Akipongezwa na katibu wa CCM wilaya ya Makete, Miraji Mtaturu kuhusu zawadi hiyo
Watumishi wa shirika la SUMASESU wakipewa mkono na mgeni rasmi
Mgeni rasmi katibu tawala wilaya Makete Joseph Chota kwa niaba ya mkuu wa wilaya, akiwapongeza wote kwa zawadi walizozitoa kama sekta binafsi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo