WALEMAVU WILAYANI MAKETE WAASWA KUACHA KUBWETEKA NA ULEMAVU WAO


 Bw. Niko Mbwilo akiongea na mwandishi wetu

Edwin Moshi, Makete
Walemavu wilayani Makete wametakiwa kutobweteka na hali ya ulemavu waliyonayo na badala yake wajishughulishe kufanya kazi mbalimbali zitakazowafaa kulingana na ulemavu walionao

Kwa kufanya hivyo kutawapunguzia hali ngumu ya maisha waliyonayo walemavu wengi wilayani hapo kwani kwa kiasi kikubwa ni wategemezi

Hayo yamesemwa na Niko Mbwilo ambaye ni mlemavu anayejishughulisha na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na miti aina ya mianzi wakati akifanya mahojiano na mtandao huu

Niko akiwa kazini
Mbwilo amesema ulemavu unatofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine, hivyo mtu anatakiwa kuangalia ni kazi gani itakayomuingizia kipato ambayo anaweza kuifanya badala ya kukaa na kubweteka ama kutegemea misaada mbalimbali

“Kwa mfano mimi ni mlemavu wa mguu, lakini nikaona ni bora kubuni shughuli hizi za mikono kwania sina ulemavu wa mikono, hivyo nafanya kazi kulingana na jinsi nilivyo, hivyo nadhania kila mlemavu akiliangalia hilo nafikiri maisha yaoa yatakuwa na unafuu”alisema Mbwilo

Amesema ingawa kuna changamoto anazokutana nazo wakati wa kufanya kazi yake ikiwemo umbali wa kufuata mitia aina ya mianzi anayoitumia kutengenezea kazi yake, uchakavu wa jingo analofanyia biashara pamoja na ugumu wa soko lakini hakati tamaa kwa kuwa shughuli hiyo ndiyo inayomuingizia kipato kwa ajili yake na familia

Malighafi anayotumia Niko
Ameongeza kwa kiasi kikubwa bidhaa anazotengeneza huwa zinategemea wateja wa nje ya wilaya ya Makete kwa kuwa wanaotengeneza bidhaa kama hizo ni wengi

Baadhi ya bidhaa anazozitengeneza ni nyungo, vikapu, viti, meza, ambavyo anavitengeneza kwa kutumia mianzi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo