Wizara
ya Ujenzi inapenda kutoa taarifa kwa Umma kwamba, Mei 22, 2013
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete atakuwa mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa miradi ya
ujenzi wa barabara kama ifuatavyo:-
1) Tarehe 22 Mei, 2013 Asubuhi kuweka jiwe la msingi sehemu ya Dodoma – Fufu Escarpment (km 93.8) katika eneo la Dodoma Mjini.
2) Tarehe 22 Mei, 2013 Mchana kuweka jiwe la msingi sehemu ya Fufu Escarpment – Migori (km 70.9) na Migori – Iringa (km 95.3) katika Kijiji cha Migori Wilayani Iringa Vijijini.
Barabara
ya Iringa - Dodoma ni sehemu ya barabara muhimu ijulikanayo kama “Great
North Road” inayoanzia Capetown Afrika ya Kusini hadi Cairo, Misri
kupitia Tanzania. Nchini Tanzania inaunganisha Miji ya Tunduma (mpakani
na Zambia), Mbeya, Iringa, Dodoma, Arusha na Namanga (mpakani na Kenya).
1) Tarehe 22 Mei, 2013 Asubuhi kuweka jiwe la msingi sehemu ya Dodoma – Fufu Escarpment (km 93.8) katika eneo la Dodoma Mjini.
2) Tarehe 22 Mei, 2013 Mchana kuweka jiwe la msingi sehemu ya Fufu Escarpment – Migori (km 70.9) na Migori – Iringa (km 95.3) katika Kijiji cha Migori Wilayani Iringa Vijijini.
Mradi huu ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara na unalenga kupanua fursa za kiuchumi na kibiashara kwa wananchi, na kati ya Tanzania na nchi jirani za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kwa njia hii, barabara itakuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Taarifa hii imetolewa na;
Balozi Herbert E. Mrango
KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI