Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal na Waziri wa Mambo ya
Nje Bernard Membe wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wapya
waliopaishwa leo ikulu jijini Dar es Salaam.aliyesimama mbele kushoto no
Balozi Liberata Mulamula anayekuwa Balozi Mpya wa Tanzania nchini
Marekani.Waliosimamanyuma kutoka kushoto ni Balozi mpya wa Tanzania
Uholanzi Wilson
Masilingi,Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Commoro Chabaka
Kilumanga,Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Geneva
Balozi Modest jonathan Mero na Balozi mpya wa Tanzania katika falme za
Kiarabu(UAE)Mbarouk Nassor Mbarouk.Kabla ya uteuzi Balozi Liberata
Mulamula alikuwa msaidi wa Rais Masuala ya kidiplomasia na aliwahi kuwa
katibu mkuu wa nchi za Maziwa Makuu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
leo ikulu jijini Dar es Salaam amemwapisha Jaji Aloycius Mujuluzi kuwa
Mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria pamoja na mabalozi wanne
watakaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.Mabalozi walioapishwa leo ni
pamoja na Balozi mpya katika umoja wa Falme za kiarabu(UAE) Mbarouk
Nassor Mbarouk,Balozi mpya wa Tanzania nchini Uholanzi Wilson
Masilingi,Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Commoro Chabaka
Kilumanga na Mwakilishi wa kudumu Tanzania Umoja wa mataifa Geneva
Balozi Modest Jonathan Mero.Picha na Freddy Maro-IKULU