PICHA ZA KANISA LILILOLIPULIWA KWA BOMU LEO ARUSHA HIZI HAPA

Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia leo asubuhi wakati wa misa ya kuzindua kigango hicho.iliyo katika kata ya olasiti na parokia ya burka
Majeruhi wa tukio hilo wakiwa katika hali mbaya.

Umati wa  wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya thelathini na watano wapo hospitali huku kukiwa hakuna taarifa ya vifo.
 Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja  amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.
 Waumini  pamoja na baadhi ya wanacchi wakiwa katika hali ya taharuki  wasiamini nini kilichotokea  kutokana na mlipuko mkubwa  uliotokea asubuhi ya leo.
Polisi waki imarisha doria eneo la tukio   baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali kupatiwa matibabu zaidi ...Mpaka tunaondoka eneo la tukio Viongozi mbali mbali akiwemo mmbunge wa arusha walikuwemo eneo hilo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo