MBUNGE WA CHADEMA AUGUA GHAFLA, ALAZWA HOSPITALI

MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mwanamrisho Taratibu Abama leo asubuhi aliugua ghafla katika viwanja vya Bunge na kukimbizwa hospitali.
 
Tukio hilo lilitokea wakati akienda  kuhudhuria semina ya wabunge kuhusu Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia kabla ya kukosa nguvu na kusaidiwa na wenzake kumkimbiza kwenye zahanati ya Bunge.
 
Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza bungeni, gari la wagonjwa lilimkimbiza Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) ambako amelazwa. 
 
Kwa mujibu wa waliomshuhudia,  alianza kuishiwa nguvu hali ambayo waliokuwa karibu walimsaidia kumpeleka kwenye zahanati ambako alitundikiwa dripu kabla ya kupelekwa hospitalini. 
 
Kaimu Mganga Mkuu wa  Hospitali ya Dodoma, Zainabu Chaula alikiri kumpokea mbunge huyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo