Watuhumiwa wa uchochezi dhidi ya
machinga wa mbunge mchungaji Peter Msigwa akitolewa mahakamani kwa
ulinzi mkali kupelekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana leo
Watuhumiwa wa kesi ya uchochezi wa
vurugu dhidi ya Machinga eneo la mashine tatu wakifikishwa mahakamani
leo kujitu kesi ya tuhuma za uhamasishaji wa vurugu inayowakabiri
,baada ya watuhumiwa hao kudaiwa kuwahamasisha machinga kufanya
vurugu jana eneo hilo la mashine tatu ambalo kisheria halitakiwi
kufanya biashara
Ulinzi ulivyoimarishwa katika mahakama
hiyo ya Mwanzo bomani leo wakati watuhumiwa hao wakifikishwa
mahakakani japo hakukuwa na mtu yeyote aliyefika kwa ajili ya
kuwatazama ama kuwadhamini watuhumiwa hao
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa
...........................................................................
Na Francis Godwin
KAULI ya mbunge wa jimbo la Iringa
mjini mchungaji Peter Msigwa ya kuwataka machinga kuvunja sheria ya
mipango miji na kufanya biashara maeneo yasiyoruhusiwa imeanza
kuwatokea puani machinga hao baada ya vijana wanne kufikishwa
mahakamani leo na kukosa mtu wa kuwadhamini.
Vijana hao wanne wamepandishwa mahakamani leo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo bomani mheshimiwa Alois Masua wakikabiliwa tuhuma ya kuhamasisha mgomo kesi namba 154 ya mwaka 2013 .
Waliofikishwa mahakamani ni pamoja na
Daniel Awadhi (35) mkazi wa Mkwawa , Petro Lupembe (20)mkazi wa
Mwembetogwa , Baraka Muhame(32) mkazi wa Ipogolo, na Joseph Chengula
(34) mkazi wa Mkwawa .
Watuhumiwa hao kwa pamoja wanashtakiwa
kwa kosa la kuhamasisha mgomo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo
maarufu kama Machinga katika eneo la Mashine tatu.
Imeelezwa mahakamani hapo kuwa
watuhumiwa hao kwa pamoja walikamatwa eneo la Mashine tatu jana majira
ya saa 4 asubuhi wakiwa na mabango yenye jumbe mbali mbali kwa ajili
ya kuhamasisha wenzao kufanya mgomo kupinga kuzuiwa kufanyabiashara
katika eneo hilo la Mashine tatu ambalo kisheria haliruhusiwi ila
mbunge wao mchungaji Msigwa aliwaruhusu kulitumia.
Hivyo kutokana na sheria kutoruhusu
eneo hilo kufanyabiashara watuhumiwa hao huku wakitambua kufanya
hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria namba 74(1)(2) kifungu cha kanuni ya
adhabu sura ya 16R;E 2002.
Watuhumiwa hao wamekana kosa
lililowafikisha mahakamani hapo huku mtuhumiwa mmoja Petro Lupembe
akiwaruka wenzake kuwa yeye kosa lake kubwa ni kutuhumiwa wizi na
wananchi wenye hasira kali ndio ambao walimkamata na kumpa kichapo
kiasi cha kuumizwa vibaya na wakati akikimbia kuuwawa na wananchi
ndipo alipokamatwa na polisi hivyo kuiomba mahakamani hiyo kumuengua
katika kesi hiyo ya machinga.
Hata hivyo mahakama hiyo haikuweza
kusikiliza utetezi wa mtuhumiwa huyo hasa ukizingatia kuwa kesi hiyo
ilikuwa ikifikishwa kwa ajili ya watuhumiwa kusomewa mashtaka yao .
Hakimu wa mahakama hiyo Mheshimiwa
Masua alisema kuwa dhamana kwa watuhumiwa hao ipo wazi kwa kila
mmoja kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Tsh
500,000 kila mmoja.
Watuhumiwa hao wamekosa wadhamini na wamerudishwa mahabusu hadi Mei 20 kesi hiyo itakapotajwa tena.
Hata hivyo katika hali ya
kustaajabisha ni baada ya kukosekana kwa mbunge wao mchungaji Msigwa
wala msaidizi wake katika mahakama hiyo wakati chanzo cha vijana hao
kukamatwa ni kutekeleza agizo la mbunge wao la kuwataka wavunje
sheria.