UONGOZI
wa Clouds Media Group kwa kupitia Mkurugenzi wao wa Utafiti na Matukio,
Ruge Mutahaba, umemtaka msanii wa Bongo Fleva, Judith Wambura, Lady Jay
Dee ajipange na kupokea changamoto badala ya kutafuta mahali kwa
kujiegemeza kwa kueneza matusi kwao.
Clouds
Media leo wamefungua mdomo kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miezi
mitano tangu Jay Dee alipokuwa akiwarushia makombora kwa madai kuwa
wameharibu soko la muziki wa Bongo Fleva sambamba na kuitangaza bendi ya
Skylight kwa ajili ya kuiangamiza Machozi Bendi.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam ambapo pia alikuwa akirushwa moja kwa moja
katika redio ya Clouds FM, Mutahaba alisema Jay Dee amekuwa akilalamikia
mambo mawili ambayo ni bendi ya Skylight na matangazo yake
yaliyoshindwa kurushwa hewani japo alilipia Sh 240,000.
Alisema suala hilo walilimaliza baada ya kumueleza kuwa redio yao haiwezi kukataa matangazo kwakuwa ndiyo wanayowafanya waendelee kuwa kinara katika suala zima la kuiendesha Clouds FM.
“Nilimwambia
kamwe hatuwezi kukataa matangazo na kama kuna lolote limefanyika, basi
ni kwa bahati mbaya, ukizingatia kuwa tayari alishafanya kazi nyingi
pamoja na kupewa urahisi kwenye kazi zake kwa kupitia Clouds FM.
“Pamoja
na yote hayo, bado matusi na kejeli yaliendelea hasa katika mitandao ya
kijamii jambo lililotufanya tuamuwe sasa kujibu japo hapo kabla
tuliamua kubaki kimya kwa ajili ya kulinda hadhi ya kazi zetu,” alisema.
Kuhusu
shutuma za kuitangaza zaidi Skylight Bendi, Ruge alisema bendi hiyo si
mali ya Joseph Kusaga, Mkurugenzi wao wala yeye, kama madai hayo
yanavyotolewa bila kufanya utafiti, isipokuwa ni mali ya Sebastian
Ndege.
“Kama
kuna mvutano kati ya Machozi Bendi na Skylight basi ni wa kibiashara
maana wote wanalipa fedha za matangazo na kama chanzo ni Jay Dee kuporwa
wanamuziki wake, hilo si jambo geni kwenye muziki.
“Dada
yangu Asha Baraka asingekuwa makini angelia sana, maana kila bendi
inayoanzishwa au kuendeshwa lazima ichukuwe wanamuziki kutoka kwake,
ukizingatia kuwa ni jambo la kawaida hivyo tumuomba Jay Dee atumie
busara katika hili pamoja na kuumiza kichwa kupokea ushindani na
changamoto kama hizo za kuchukuliwa wanamuziki,” aliongeza Ruge.
Aidha,
Ruge alisema Clouds FM ni redio ya watu binafsi, hivyo si ina utaratibu
wake katika utendaji wa kazi, ikiwapo kuchagua nyimbo au kuacha kupiga
kama kuna mtu amekwenda kinyume, hasa wale wanaopita nje na kuanza
kuwatusi, kuwakejeli bila kukumbuka fadhira walizofanyiwa kabla ya kuwa
maarufu wao.
Pia
alisema Clouds FM ipo tayari kufanya majadiliano ya wazi na mtu yoyote
mwenye hisia tofauti juu yao, huku ikiwataka wasanii waongeze bidii
katika kazi zao ili wasimlaumu mtu wanapoanguka na kuwapisha wengine,
maana muziki unaonekana ni wa kupokezana vijiti.
Katika
siku za hivi karibuni katika vyombo vya habari hasa hasa kwenye
mitandao ya kijamii nchini kumekuwa na taarifa rasmi na zisizo rasmi
kutoka kwa Mwanamuziki Lady Jaydee alilalamikia Kituo chetu cha Clouds
FM na wakurugenzi wake Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga.
ENDELEA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPO CHINI.