MARUFUKU MACHINGA KUREJEA MASHINE TATU IRINGA

 
Na Francis Godwin
Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Bi.Terresia Mahongo (pichani) amesema  kuwa  ni marufuku machinga  kufanya  shughuli  zao katika  eneo la barabara  ya Mashine  tatu ambalo kisheria haliruhusiwi kutumika kwa  shughuli  hizo.
 
Kauli  ya  mkurugenzi  Mahongo imekuja  ikiwa ni  siku  mbili tu zimepita  baada ya  mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa  (Chadema)  kuwahamasisha machinga   kupitia mkutano  wa hadhara  kurejea  eneo  hilo kesho  jumapili.
 
Kwa  mujibu  wa Mahongo  kuwa   maamuzi ya  kuwaondoa machinga  eneo hilo yalifanyika na baraza la madiwani hivyo hatua ya  machinga  hao  kurejea  eneo hilo ni uvunjaji  wa  sheria.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo