MAHAKAMA YAMUACHIA HURU RAMA ALIYEKUTWA NA KICHWA CHA MTU

Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeamua kumuachia huru Ramadhani Selemani Mussa ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na kichwa cha mtu. 
 
Rama, ambaye muda wote huo alikuwa rumande gereza la Segerea akisota kusubiri hukumu yake, alikamatwa hospitali ya Muhimbili mwaka 2008 ambapo pia alikiri kuwa alikuwa na tabia ya kula nyama za watu ambayo amefundishwa kichawi toka alipokuwa mdogo. 
 
Mahakama imemuachia huru kwasababu mtuhumiwa alitenda kosa hilo pasipo kuwa na akili timamu. 
 
Hata hivyo mahakama hiyo imetoa agizo la kuendelea kumuweka kijana huyo katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili, hospitali ya Isanga iliyopo Dodoma mpaka pale atakapona ndipo aruhusiwe kurudi mtaaani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo