MAGARI YA KWAMA BARABARA YA DHARURA MOMBO MKOANI TANGA

TAKRIBAN saa moja mabasi na magari mengine ya mizigo makubwa kwa madogo yaliyokuwa yakitumia barabara kuu ya Mombo –Same yakitoka Arusha, Moshi  kwenda Dar es Salaam na Mengine Mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Morogoro kuelekea Arusha yalikwama katika eneo la Mombo Mkoani Tanga kufuatia kunasa katika shimo kwa gari la Mizigo aina ya Fusso.

Juhudi za kulinasua gari hilo zilifanywa baina ya madereva na wakandarasi wanaojenga barabara hiyo Kampuni ya Strabag ya Ujerumani na kufanikiwa kuleta moja ya magreda yake na kulivuta gari hilo.

Baada ya kulitoa gari hilo mafundi wa kampuni hiyo walimwaga kifusi katika eneo hilo ambalo limeharibika vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha nchini kote.

 Baadhi ya abiria wakiwa chini wakitafakari namna ambavyo wataweza kupita eneo hilo.
 Maofisa wa Kampuni ya Strabag wakijadiliana jambo wakati zoezi la kulinasua gari hilo likiendelea.
 Abiria wakiwa hawana la kufanya..
 Gari hilo aina ya Fusso likiwa limekwama..
 Eneo ambalo lilikwama gari hilo...
 Nyororo ikifungwa tayari kulinasua gari hilo.
 Hili nalo lilikwama na kusukumwa kidogo..
Abiria wakirejea katika mabasi yao kuendelea na safari...PICHA ZOTE NA FATHER KIDEVU


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo