KUFUATIA KANISA KULIPULIWA ARUSHA, ASKOFU DKT MDEGELLA ATAKA MAKANISA KULINDWA



NA FRANCIS GODWIN
Kufuatia shambulio la  kulipuliwa  kwa kanisa katoliki la Olasit nje kidogo ya mji wa Arusha na kupelekea  watu zaidi ya 30  kujeruhiwa na mmoja  kusadikika kupoteza maisha yake ,askofu wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dayosisi ya Iringa Dkt Owdenburg Mdegella amesema  kuwa  wanafanya  hivyo ni watu  ama mtu anayetaka  kuvuruga amani ya Tanzania na kutaka  nyumba zote za ibada  kuwa na ulinzi .

Askofu Dkt Mdegella ametoa kauli  hiyo leo  wakati akizungumza katika mahojiaono maalum na mtandao huu kuhusiana na tukio la kulipuliwa kwa kanisa mkoani Arusha.

Kwani  alisema  alishapata   kukutana na vyombo  vya habari  kufuatia tukio la kuchomwa kwa kanisa Zanzibar na  tukio la  kuuwawa kwa  Paroko  kwa  risasi  huko  huko  Zanzibar ila ushauri  wake  alioutoa kwa  serikali  kuwa  hivi  sasa  nchi  inakundi la watu  wanaoendesha ugaidi ,na  kutaka  vyombo  vya  usalama  kusaidia  kupambana na kundi  hilo.

Kwani  amesema  kuwa hivi  sasa  amani ya Taifa  inazidi  kuwa hatarini zaidi  kutokana na watu hao  wanaoendesha  vitendo vya  kigaidi  kuingia kwa kasi kubwa  kushambulia makanisa na kuwa  ni vema  vyombo  vya ulinzi na usalama  kusaidia  kulinda  nyumba  za ibada ili  kunusuru njama  hizo  za  kigaidi.

Mbali ya  kuvitaka  vyombo  vya usalama  kusaidia  kulinda makanisa  bado alishauri  waumini wa  makanisa  hapa nchi kuwa makini  zaidi na ikiwezekana  kuongeza  ulinzi zaidi katika makanisa  yao hasa  siku za ibada  .

Askofu  Dkt  Mdegella alisema  kuwa  yawezekana  ni kundi la  watu  wanaotumia ugaidi kuhatarisha amani ya  Tanzania  ila  pia yawezekana mambo  haya ya machafuko  yanafanywa na  kundi furani la kisiasa  kwa lengo la  kuichafua  serikali ya  CCM iliyopo madarakani kama njia ya kuchinganisha umma kuona kama Rais Jakaya  Kikwete na chama  chake nchi imemshindwa jambo ambalo halipaswi kuungwa mkono na mtanzania yeyeto kwa  watu kuchafua amani ili  wapate  kuingia Ikulu.

Bila  kutaja  jina la chama  cha  siasa kinachofanya  hivyo wala  mtu anayefadhili vitendo  hivyo vya kigaidi askofu Dkt Mdegella aliwataka  wana  siasa na  wananchi  kuwa  kitu  kimoja katika kulinda amani ya Taifa hili.

 Pia  aliulaumu  uongozi  wa kanisa  Katoliki Arusha  kwa  kushindwa  kuimarisha  ulinzi kwa  siku ya Jana ambapo  walitambua  wazi  wana tukio  kubwa na tayari  kumekuwepo na vitisho  mbali mbali na  kuwa  iwapo  ulinzi  ungewekwa  eneo hilo yaliyotokea  huenda  yasingetokea.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo