Baadhi ya wasanii wa filamu Bongo, kutoka kushoto ni: JB, Ray, Uwoya, Richie na Wema.
Na Imelda MtemaTAMASHA la Filamu Zanzibar (ZIFF) limewataka wasanii mbalimbali wa filamu kupeleka filamu zao ili zikaguliwe mapema kuepusha lawama ukifika wakati wa kutoa tuzo.
Akizungumza na Stori 3, mratibu wa tamasha hilo, Hassan Bond ‘Hazt’
amesema wasanii wengi kila mwaka wamekuwa wakitoa lawama kuwa hawakupewa
taarifa mapema hivyo mwaka huu wameanza kuwataarifu mapema.
“Tunahitaji kazi zije kwa wingi, tuzikague ili kuzithibitisha kabla tamasha halijaanza kuunguruma miezi kadhaa ijayo,” alisema Hazt.