JACQUELINE WOLPER KUMUENZI MAREHEMU KANUMBA

Na Imelda Mtema
STAA daraja A ndani ya Bongo Movies, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa anatarajia kumuenzi marehemu kwa kuachia vipande vya filamu ya After Death ambayo ni mwendelezo wa filamu ambayo ilichezwa na marehemu Steven Kanumba, Uncle JJ.


Akipiga stori na paparazi wetu, Wolper alibainisha kuwa anatarajia kuonesha vipande vya filamu hiyo katika siku ya Kumbukumbu ya Kanumba itakayofanyika Aprili 7, mwaka huu katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar.

“Ni filamu ambayo nimeiandaa katika mazingira maalum kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba ambaye kila Mtanzania anatambua mchango wake kwenye sanaa,” alisema Wolper.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo