Wakazi
wa maeneo ya Kibamba, Mbezi na Kimara jijini Dar es Salaam wanaotumia
barabara ya Morogoro kuelekea maeneo yao ya kazi leo wamejikuta katika
wakati mgumu baada ya kushindwa kufika kazini kwa wakati kutokana na
msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo.
Baadhi ya watumiaji wa barabara hiyo wameiomba kampuni ya ujenzi ya STRABAG inayoendesha ujenzi huo kufanya kazi zake nyakati za usiku ili kupunguza adha kwa watumiaji wengine wa barabara.
Msongamano huo wa magari umekuwa neema kwa madereva wa pikipiki wanaobeba abiria maarufu kama bodaboda ambao wamejipatia abiria kwa wingi waliokuwa wakiwahi kazini na kukwepa msongamano huo.