TAARIFA MUHIMU KUTOKA TFF

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
...............................................
Semina elekezi kwa ajili ya michuano ya Copa Coca-Cola 2013 iliyokuwa ifanyike Jumanne (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam sasa imesogezwa mbele hadi Machi 26 mwaka huu.

Afisa habari  wa TFF Boniface Wambura Mgoyo amesema  kuwa Uamuzi wa kusogeza mbele semina hiyo umetokana na maombi ya wadhamini, Coca-Cola ambao katika tarehe ya awali watakuwa na shughuli nyingine za kampuni hiyo.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi wajumbe kwa usumbufu wowote utakaokuwa umejitokeza kutokana na semina hiyo kusogezwa mbele.

Hivyo, washiriki wa semina hiyo wanatakiwa kuripoti Dar es Salaam (TFF) siku moja kabla (Machi 25 mwaka huu).

Washiriki hao ni makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar. Pia waratibu wa mikoa wa mashindano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).

Barua za mwaliko kwa ajili ya semina hiyo tayari zimetumwa kwa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo