Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Meneja wa Baraza la Habari kanda ya Zanzibar Suleiman Seif
Omar ( Bin Seif) amewataka waandishi wa habari kufanya utafiti wa kina
katika habari wanazoziandika kama zina ukweli na uhakika.
Hayo aliyasema jana wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali katika ukumbi wa Mansoon Hotel Vuga
Alisema waandishi wa habari wanapokuwa kazini wawe makini
kuandika habari zinazozingatia maadili yote ya habari ikiwemo ukweli na
uhakika.
Alisema kuandika habari kwa kuzingatia vigezo hivyo kunamuwezesha mwandishi kuwa muadilifu na kujiamini katika kazi yake.
Alisema Baraza la Habari Tanzania kazi yake ni kushajihisha
waandishi wa habari na kuiwapa muongozo jinsi wa utafutaji wa habari na
kuziandika vyema ili ziwafikie wananchi wa taifa hilo .
“Kila mtu ana haki ya kupata habari ila habari hizo ziwe za
ukweli na uhakika hivyo mwandishi nalazimika kuzifanyia utafiti wa kina
habari anazozipata kabla ya kuziwasilisha kwa wananchi kupitia chombo
cha habari”. Alisisitiza Bin Seif.
Meneja huyo aliwaambia waandishi wa habari wawe watafiti wa
habari na matukio ili kuziwasilisha kwa wananchi kama tukio hilo
lilivyotokea.
Nae mwandishi wa BBC Ali Saleh (Alibato ) alisema kuwa
waandishi wa habari wanatakiwa kujifunza zaidi ili kuepukana na makosa
ambayo hayastahiki kujitokeza na kuitia aibu fani hiyo.
“Habari zipo lakini waandishi wa habari hakuna kutokazana na
kutoweza kujifunza kusoma makala, vitabu pamoja kutosikiliza habari
mbali mbali za ndani na nje ya nchi”. Alisema Ali Saleh.
Nao waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo walisema
hakuna uhuru wa kutosha katika kutoa habari jambo ambalo linawajengea
hofu na kutokujiamini katika kazi zao .
Mkutano huo wa siku moja kwa Waandishi wa Habari
umeandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) ambao umebeba mada Haki
ya Kupata Habari