Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba akihojiwa na
mwandishi wa habari wa TBC Grace Kingalame wakati alipotembelea eneo la
tukio na kujionea hali halisi ya uokoaji.Picha na John Bukuku
---
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba
alitumia fursa hiyo kuitaka Serikali kuwabana makandarasi wasio na sifa
kwani wanahatarisha maisha ya watu.
“Huu ni uzembe, wahandisi wa jiji walikuwa wapi? Wasimamizi na washauri walikuwa wapi hadi jengo linafikia ghorofa 16?” Alihoji Profesa Lipumba.
Profesa Lipumba aliitaka Bodi ya Makandarasi (CRB)
kufuta leseni ya kampuni hiyo, kwani imeonyesha kuwa haiwezi kusimamia
ujenzi na hivyo kusababisha vifo