
WANAWAKE watatu raia wa Rwanda
wanaosadikiwa kuendesha biashara ya ukahaba mjini Dodoma wamekamatwa na
kupewa siku tatu kuondoka nchini, huku wawili kati yao wakikutwa na
vidonge vya kupunguza makali ya virusi ya Ukimwi (ARVs).
Kulingana na maelezo yao,
Esperance alitangulia kuja nchini kisha kuwaita wenzake ambao ilikuwa ni
mara ya kwanza kuja nchini, lakini hata hivyo alisema kuwa, kumekuwa na
makundi ya wanawake kutoka Rwanda wanaokuja nchini kipindi cha Bunge na
hata mwaka jana kuna kundi lilikuja wakati wa mkutano wa Halmashauri
Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kukamatwa kwa wanawake hao ambao
ni Esperance Hagenimana (28), Vestina Zaninika (27) na Ziada Mukamurera
(25), kunafuatia mmoja wao Esperance kwenda kutoa taarifa kituo cha
polisi kuwa alikuwa ameibiwa fedha taslimu Sh 800,000 na hati ya
kusafiria.
Lakini, Polisi walipofika nyumba
ya kulala wageni waliyofikia iliyopo eneo la Area D walikuta wanawake
wengine wawili ambao walikuwa wakikaa chumba kimoja na Esperance.
Uchunguzi wa Polisi ulibaini
kuwa mwanamke huyo hakuibiwa na kubaini wote si raia wa Tanzania. Hata
hivyo kilikosekana kifungu cha kuwashitaki ndipo waliamua kupeleka
sakata hilo Uhamiaji ili liweze kushughulikiwa.