PAPA MPYA APATIKANA, NI CARDINAL JORGE MARIO BERGOGLIO KUTOKA ARGENTINA

Moshi mweupe ukiashiria kupatikana kwa papa mpya

Waumini wa kanisa Katoliki  duniani wamepata kiongozi mpya Baada ya makadinali kukutana katika kikao cha siri na kufanikiwa kumchagua Pope mpya  CARDINAL JORGE MARIO BERGOGLIO (umri miaka 76) wa Argentina.


Umati wa maelfu ya waumini wa madhehebu ya Kikatoliki wamekusanyika katika uwanja wa St.Peter's Square huko Rome wakishangilia baada ya kuona moshi mweupe ukifuka juu kuonyesha ishara ya kuwa Makadinali wamemchagua Papa mpya. Dakika chache baadaye akajitokeza.

Katika wadhifa huo atajulikana kama Papa Francis.

Yeye  ni Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo