Mwili wa Vumilia ukiwa chini baada ya kuanguka juu ya mti leo
NA FRANCIS GODWIN
Mkazi wa Mwangata B katika Manispaa
ya Iringa Vumilia Sanga (35) amepoteza maisha yake leo jioni baada ya
kuanguka kutoka juu ya mti wakati akichuma matunda aina ya mapera nje
ya nyumba yake .
Tukio hilo limetokea jioni ya leo
majira ya saa 10 baada ya mwanamke huyo ambae anasadikika kuwa alikuwa
akishumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa.
Wakizungumza na mtandao huu leo wakazi wa eneo hilo wakiwemo
ndugu wamedai kuwa kabla ya kifo chake marehemu alikuwa
akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa na inawezekana tatizo hilo
lilimkuta akiwa juu ya mti huo na hivyo kuanguka na kuchomwa na mti
mgongoni na kutokea tumboni .
Alisema mkazi wa eneo hilo
alijitambulisha kwa jina la Adam Kalinga kuwa kutokana na mwanamke
huyo kuanguka juu ya mti majirani walijaribu kutaka kumwokoa ila
baada ya kusogea walikuta tayari utumbo na maini yakiwa nje na
kabla hata ya kumgusa alikata roho .
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wa
mwangata B Julius Lwimbo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na
kuwa hadi majira ya saa 11.45 jioni polisi walikuwa bado hawajafika
eneo la tukio ili kuutoa mwili huo .
Pia mwenyekiti huyo amekiri kuwa ni kweli mkazi huyo alikuwa
akisumbuliwa na ugonjwa wa kifafa na kuwa yawezekana kuanguka kwake
kumetokana na tatizo la ugonjwa huo na kuwa baada ya kuanguka toka
juu ya mti aliangukia katika jiti ambalo lilikuwa limechongoka na
ndilo limemtoa uhai wake .