MH MBOWE AVUNJA KAMATI YA UTENDAJI YA CHADEMA WILAYA YA TARIME

Mwenyekiti wa Chademan,Mbunge wa Hai na  Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe akiongea na wajumbe wa Kamati ya Utendaji Wilaya ya Tarime na madiwani.Picha na Habari na CHADEMA

Baada ya kikao cha ndani kati ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji Wilaya ya Tarime na madiwani, kubaini udhaifu wa kiuongozi ulioruhusu kuzuka kwa makundi yaliyokuwa yakidhoofisha utendaji kazi na uhai wa chama wilayani hapa, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amevunja uongozi wa wilaya hiyo (kwa maana ya Kamati ya Utendaji).

Uamuzi huo uliofanyika jana mchana, ulipokelewa kwa mikono miwili na wajumbe wa kikao hicho.

Baada ya kikao hicho cha Kamati ya Utendaji na madiwani wa CHADEMA Wilaya ya Tarime, Mwenyekiti Mbowe alikutana na wanachama na wadau wa chama wa Tarime, kwenye kikao cha ndani, ambapo kwa kauli moja waliupokea kwa furaha uamuzi huo wa kuvunjwa kwa uongozi huo, huku wakiomba nafasi hizo za uongozi zijazwe mapema kwa ajili ya kuendelea kukiimarisha chama.

Uongozi wa chama katika ngazi za kata hadi misingi utaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Kwa hatua hiyo, uchaguzi wa kupata uongozi wa Kamati ya Utendaji ya muda, utafanyika ndani ya mwezi mmoja ukisimamiwa na ngazi ya juu

Mwenyekiti Mbowe amewataka watu wa Tarime kutopoteza ari yao ya dhati katika kukisimamia na kukipigania CHADEMA katika kuendesha mapambano ya ukombozi wa pili wa nchi, ambayo ilikuwa ni mfano wa kuigwa wa wanaChadema nchi nzima, kiasi cha watu kusalimiana..."mambo...kama Tarime..."
Habari nimeihamisha kutoka hakingowi.blogspot.com


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo