FILAMU YA BIKIRA KIDAWA YAINGIA SOKONI

Ruth Suka
Mainda mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

HATIMAYE filamu mpya ya kimataifa ya Bikira Kidawa imeingia sokoni kwa kishindo baada ya kuzikimbiza filamu zilizpo mtaani Mtayarishaji wa filamu na mwandishi wa muswada, Octavian Natalis ‘Mdau Octa’ ameeleza kuwa, sinema hiyo imeingia sokoni mwishoni mwa wiki iliyopita.

Zubery Mohamed
Niva mshiriki wa filamu ya Bikira kidawa .
Ruth Suka
Mainda akiwa katika pozi!
Filamu Kidawa
Filamu ya Kidawa

“Filamu ipo sokoni tangu Ijumaa ni wakati wa watazamaji kujionea filamu bora ya Bikira Kidawa,” alisema Octavian.

Akiizungumzia filamu hiyo, alieleza kuwa ni moja ya filamu zinazoelezea hali halisi ya Mtanzania wa kawaida, ikielimisha kuhusu ubaya wa mila potofu, mimba za utotoni, wazazi kutengana, malaria na Ukimwi.

Baadhi ya waigizaji waliotamba ndani ya Bikira Kidawa ni Janet Lameck aliyeigiza kama kinara, Zubeir Mohamed ‘Niva’, Ruth Suka ‘Mainda’, Mohamed Fungafunga ‘Jengua’, Korongo Hamis Korongo, Shamila Ndwangila ‘Bi Staa’, Abdallah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’, Fatma Abubakari na muigizaji aliyetamba na sinema ya Laptop, Hamida Atos pamoja na waigizaji wengine lukuki.

Filamu hiyo imepigwa picha na kuhaririwa na Suleiman Omar ‘Suleish Marah’ na kuongozwa naRashid Mrutu aliyewahi kuongoza filamu za Gongolamboto na Laptop. 

Imeandikwa muswada na Octavian Natalis aliyewahi kuandika filamu za Sanda Nyeusi, Kesi ya Jinai (Babu Seya), Kimya, Albino Mgeni, Gongolamboto na Laptop. Zaidi ya wasanii 84 wameshiriki katika kuigiza filamu ya Bikira Kidawa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo