BAVICHA KYELA WAMTWANGA BARUA AFISA ELIMU, KISA ELIMU INASHUKA



CDM/BAVICHA/2013/1.
                      BARAZA LA VIJANA CHADEMA (BAVICHA),
                                                                       CHADEMA WILAYA,
           P.O BOX 599,
   KYELA.
      25/02/2013
                    SIMU:0712 725 444
AFISA ELIMU (W) KYELA,
P.O BOX
KYELA.
25/02/2013

Kamati ya taarifa na ufuatiliaji kyela iliyojumuisha wanazuoni wa kyela na wajumbe  toka katika wilaya ya Kyela  iliyoteuliwa na BAVICHA siku ya jumamosi Tarehe 23/02/2013 chini ya kamati kuu, chini ya chama cha  CHADEMA wilaya ya Kyela iliamua kuja kuhoji na kutoa matamko leo Jumatatu tarehe 25/02/2013 kwa Afisa Elimu Wilaya, kamati inamtaka Afsa Elimu wa Wilaya kujibu mambo yaliyoainishwa na kuazimiwa na kamati kuhusu suala la Elimu Kyela kama ifuatavyo;-
1.      Afisa elimu anatathimini vipi kushuka kwa kufaulu kwa wanafunzi? na ni kwasababu zipi zinapelekea kukithili kwa kufeli kwa wanafunzi hao? Ngazi ya;
v  Darasa la saba
v  Kidato cha pili
v  Kidato cha nne
2.      Ni hatua gani zinachukuliwa na ofisi yako kuthibiti kufeli kuliko kithili kwa wanafunzi?ni zipi hatua za haraka (immediate solutions) na za muda mrefu (long-term salutions)?
3.      Fedha za malipo kwa walimu wa muda(part time-form six leaver na wahitimu wa vyuo vikuu) ,zinalipwa kwa flat rate ya Shilingi ngapi kila mmoja?na ni vigezo vipi vya malipo vinavyotumika?na Ofisi yako inatenga Shilingi ngapi kwa ajili ya waalimu hao?
4.      Kwanini baadhi ya shule zinakataa kuwapokea walimu wa mafunzo kwa vitendo(field)kwa kuzingatia vigezo visivyo na muhimu kwa mfano, eti walimu kutoka UDSM watasababisha migomo kwa wanafunzi?na Kyela day ikiwa moja ya shule iliyotoa tamko hilo,ofisi yako ilichukua hatua gani?na inampango gani kwa walimu hawa?
5.      Ni mpango upi mkakati unaotoa mwelekeo wa kuleta umeme mashuleni?ikizingatiwa shule kama Nkuyu,nguzo zipo karibu kabisa,tatizo ninini?
6.      Je kuto kuwepo kwa vitabu vya kiada(Basic books) mashuleni ni hatua zipi madhubuti zinazochukuliwa na ofisi yako ili kuleta vitabu hivyo mashuleni?na ni hatua zipi zinachukuliwa kudhibiti kuenea kwa vitabu vya ziada vinavyotumika kufundishia mashuleni?
7.      Je wanafunzi waliofeli, ni mpango upi madhubuti ambao Ofisi yako imeweka wa kuwafanya wanarudi shule,ili kuondoa kundi kubwa la vijana wasio na elimu ya kutosha kutokana na kufeli kwao?
8.      Je ni utaratibu upi unaotumika kudhibiti masomo ya ziada(tutions) ikizingatiwa wanoafungua vituo hivyo kwanza hawana sifa katika kufundisha,pili hawanaithibati/mtaala na  ni  utaratibu gani unaotumika kufungua vituo hivyo?
9.      Maazimio ya wilaya juu ya uwepo wa mitihani ya Mock kwa kidato cha tatu kama kipimo na kigezo cha  kumfanya mwanafunzi arudi darasa akifeli,je maazimio hayo yanafuatwa?je upangaji wa fedha za mitihani hiyo zilijumuisha vitu gani na kwa vigezo vipi?je ni kwa kiasi gani wazazi wanafahamu juu ya maazimio hayo ?na kama hakuna matokeo tarajiwa(impact) kwa mitihani hii,kuna umuhimu gani wa uwepo wa mitihani ya mock kwa kidato cha tatu?wito wa kamati, kama uwepo wa mitihani ya mock ni lazima ni vyema maazimio hayo yafuatwe na wanafunzi waliokosa alama za maazimio hayo warudie darasa, na kama haina ulazima ni vyema mitihani hiyo ifutwe na pesa zirudishwe kwa wazazi.
10.  Je kunamitihani mingapi kwa mwanafunzi kutoka darasa moja kwenda darasa lingine, na inazingatia alama zipi?na je hizo alama zinasimamiwa?

11.  Je ubovu wa maslahi ya walimu likiwa kama sababu moja wapo ya kufeli kwa wanafunzi kutokana na kushuka kwa morali ya waalimu katika kufundisha,linatathiminiwa vipi na ofisi yako,na ni njia zipi madhubuti zinachukuliwa ili kutatua tatizo hili?kwa upande wa vifaa duni vya kufundushia kama nyenzo anazotumia mwalimu,je ofisi yako imechukua hatua gani kuhakikisha walimu hawa wanapata vifaa bora?hasa vitabu na vifaa vya maabara.
12.  Umbali wa baadhi ya shule kutoka majumbani,unadhibitiwaje hasa kwa shule za vijiji vya mbali na Kyela mjini,kwa mfano wanafunzi wanaotoka kijiji cha Itekenya kwenda katumba songwe sekondari ni urefu mkubwa mno,ipo mikakati ipi katika kujenga mabweni ili kuepusha mazingira hatarishi?
13.  Uchaguzi wa wanafunzi kutoka darasa la saba kwenda kidato cha kwanza alama zimeshushwa kutoka 250 miaka michache iliyo pita kwenda 70 kwasasa,je ofisi elimu wilaya haioni kuwa hiki ni moja ya kigezo cha kutengeneza wanafunzi watakao feli na kuhitimu na sifuri na si kufaulu? je kuhamisha darasa kutoka shule ya msingi na kwenda shule ya sekondari kwa mfano kutoka Nkuyu shule ya msingi kwenda Nkuyu sekondari au kutoka mbogela shule ya msingi kwenda Kyela sekondari,ofisi yako haioni kwamba inazorotesha elimu kwa kutengeneza darasa lilelile,lenye wanafunzi walewale wa alama zilezile na kufeli zaidi?
14.  Kwanini shule ya kyela sekondari inawafukuza na kuto wapa ruhusa wanafunzi wa shule nyingine za sekondari katika kutumia miundombinu hiyo ikiwamo umeme wakati wa masomo ya ziada jioni?je ofisi yako imechukua hatua gani katika kuwafanya wanafunzi hawa wapate fursa sawa za kutumia umeme huo?wanafunzi wa kyela sekondari, achilia mbali shule nyingine za sekondari hawawezi kusoma zaidi ya saa kumi na mbili jioni,je hili sio tatizo linaloongeza kufeli?kwa uhakika upi wanafunzi hawa wanaweza kujisomea wakiwa majumbani?

HITIMISHO
kutokana na matamko hayo(orders) ya mambo ya hapo juu kamati teule na huru ya BAVICHA na iliyojumuisha wanazuoni na wajumbe wengine inatoa siku mbili kuanzia jumatatu ya tarehe 25/02/2013 ifikapo jumatano ya tarehe 27/02/2013 asubuhi umma uwe umepata majibu ya kina kutoka kwa Afisa Elimu wa wilaya ya kyela na yanayokidhi (ambayo ni relevant)yenye ukweli,utashi na ubora kuhusiana na suala la elimu.Majibu ya Afisa Elimu wa Wilaya yapitie aidha vyombo vya habari au ofisi ya kamati teule ya BAVICHA  chini ya ofisi kuu chadema wilaya.kinyume na maagizo hayo NGUVU YA UMMA itatumika.

                                                  NAKALA;
                                                  MKUU WA WILAYA-KYELA.
       MKURUGENZI WILAYA –KYELA.
            M/KITI WA HALMASHAURI-KYELA.
                                                  CHADEMA WILAYA-KYELA.
 CHADEMA BAVICHA-KYELA.

____________________________                         ______________________
M/KITI KAMATI YA UFUATILIAJI,                                       KATIBU BAVICHA(W),
LUSAJO BERNARD MWAMAFUPA,                                  NSAJIGWA BONIFACE
0712 725 444/0687 725 444.                             0762 011 709/0658 290 813.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo