Hii ni habari maalum kuhusu taarifa za uhakika kuhusu yule bibi wa miaka 60
aliyeua jambazi kwa risasi Bagamoyo Pwani December 9 mwaka jana.
Stori za kuaminika ni kwamba bibi
huyu ambae anamiliki shule mbili amekimbia nyumbani kwake na sasa
hajulikani alipo, hiyo imetokana na vitisho vilivyomuandama.
Siku kadhaa baada ya kufanikiwa
kuua jambazi mmoja kati ya majambazi zaidi ya watano waliomvamia
nyumbani kwake, Bibi alisafiri kwenda nje ya nchi kwa matibabu lakini
kabla ya kurudi kwake alipata taarifa za kushtua.
Uhakika wa hizo taarifa ulionyesha kwamba kundi la watu wasiojulikana wakiwa na silaha wamekua wakimuwinda.
Bibi sasa hivi hapatikani kwenye
simu, ameicha nyumba yake ya ghorofa ufukweni mwa bahari ya hindi na
sasa anaishi kusikojulikana.
Ni bibi shupavu ambae uhodari
wake wa kutumia bastola kwa uzoefu wa mwaka mmoja jeshini ndio ulimfanya
aue jambazi moja kati ya majambazi ambayo yalivamia nyumbani kwake
December 2012, ni nyumba ya ghorofa.. na chumba cha bibi chenye sebule
yake pia kiko juu lakini ngazi za kupandia ziko nje, hakuna ngazi ya
ndani ndio maana ilikua rahisi majambazi kupanda walipoona mpango wa
kurusha risasi wakiwa chini hauna nguvu
