Na Gabriel Kilamlya
Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS Mkoani Njombe Umesema Utaweka
Mizani Katika Barabara ya Njombe Hadi Makete Ili Kuyadhibiti Magari
Yenye Uzito wa Zaidi ya Tani Kumi Ambayo Yamekuwa Yakitumia Barabara
Hiyo na Kusababisha Uharibifu wa Mara Kwa Mara.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Njombe Mhandisi Yussuph Mazana Amesema Wataalamu na Maafisa wa TANROADS Watakuwa Wakitembea na Mizani Hiyo Katika Barabara na Kupima Magari Yote Kabl ya Kuyabaini Yale Yote Yatakayokuwa Yamezidi Uzito na Kuchukua Hatua Zinazostahiki.

Hatua Hiyo ya TANROADS Inafuatia Malalamiko ya Mara Kwa Mara ya Wananchi Mkoani Njombe Hasa Watumiaji wa Barabara ya Njombe Hadi Makete Barabara Ambayo Imekuwa Ikiharibika Kutoka na Kutumiwa na Magarai Yaliozidi Uzito.
Katika Kile Kinachoonekana Kuwa ni Muendelezo wa Kero Zinazowakabili Wananchi Wanaotumia Barabara Hiyo,Hivi karibuni Zaidi ya Magari Mia Moja Yalikwama Kutokana na Hali Mbaya ya Barabara Katika Kipindi Hiki Ambacho Ukarabati Umekuwa Ukiendelea.
Baadhi ya Wananchi Pia Walilazimika Kuifunga Barabara Hiyo Kwa Saa Kabla ya Jeshi la Polisi Kufika Eneo Hilo na Kuruhusu Shughuli Nyingine.