ZAIDI YA WAFANYAKAZI 30 WA KIWANDA CHA FULANA WANUSURIKA KIFO MKOANI MOROGORO

 Picha na Maktaba
Zaidi ya wafanyakazi 30 wa kiwanda cha kutengeneza fulana cha Mazava kilichopo eneo la Msamvu manispaa ya Morogoro na kinachomilikiwa na raia kutoka China wamenusurika kufariki dunia baada ya kupoteza fahamu. Wafanyakazi hao wamenusurika kufa kufuatia kukosa hewa baada ya kutokea hitilafu ya umeme kutoka katika kiwanda hicho na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

Hitilafu hiyo inadaiwa kutokea leo majira ya saa 3 asubuhi baada ya cheche za umeme kutokea ndani ya kiwanda hicho katika baadhi ya mashine na kusababisha moshi mzito na kukosa hewa kwa wafanyakazi hao na hivyo kupelekea kupoteza fahamu.


Hata hivyo inadaiwa kuwa baada ya hayo yote kutokea uongozi wa kiwanda hicho uliwafungia wafanyakazi hao ndani ya kiwanda hicho kwa saa kadhaa kwa lengo la kuficha watu wengine wasijue kilichotokea.                                  Bofya hapo chini kumsikiliza Dkt Lyamuya


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo