
Waziri
mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akikata utepe kwa
kushirikiana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za
Atomiki Duniani Yukiya Amano (wa pili kutoka kushoto) kuashiria
uzinduzi rasmi wa jengo jipya lenye vifaa vya kisasa kwa ajili ya
kuwahudumia wagonjwa wa kansa katika Taasisi ya Kansa jana Ocean Road
jijini Dar es salaam. Wengine ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto), Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya
Kansa Ocen Road Prof. Twalib Ngoma (wa tatu kutoka kushoto) na Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid.

Waziri
mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akiwaonyesha wageni
mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa jengo jipya la kuwahudumia wagonjwa
wa kansa katika Hospitali ya Kansa Ocean Road kitabu cha Mkakati wa
Kitaifa wa Kudhibiti na kupambana na Kansa nchini.

Mkurugenzi
mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani Yukiya Amano
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es
salaam mara baada ya kuzinduliwa kwa jengo jipya la Taasisi ya Kansa
Ocean Road lililojengwa na serikali ya Tanzania huku shirika hilo
likitoa msaada wa mashine mbili kwa za kutambua athari za ugonjwa wa
kansa kwenye mwili wa binadamu.

Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)
jijini Dar es salaam mara baada ya kuzindua jengo jipya la Taasisi ya
Kansa Ocean Road lililojengwa na serikali ya Tanzania lenye uwezo wa
kuhudumia wa 257 kwa gharama ya shilingi bilioni 7.2 huku Shirika la
nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) likichangia mashine 2 za kutambua sehemu
zilizoathiriwa na ugonjwa wa kansa katika mwili wa binadamu zenye uwezo
wa kuhudumia wagonjwa 1600 kila moja kwa mwaka.

Baadhi ya
wataalam wa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road wakiwa ndani ya moja ya
chumba cha jengo jipya lililozinduliwa jijini Dar es salaam chenye moja
ya mashine yenye uwezo wa kuwahudumia wagonjwa 1600 kwa mwaka. Mashine
hiyo imetolewa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA).

Sehemu ya nje ya jengo jipya la Taasisi ya Kansa ya Ocean Road lenye vifaa vya kisasa lilozinduliwa leo jijini Dar es salaam.