Kutoka kulia Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Assah Mwambene, mwanahabari mkongwe Jenerali Ulimwengu, na Mohamed Abulrahaman kutoka idhaa ya kiswahili ya DW
Washiriki wakiwa nje baada ya mdahalo kumalizika
======
Uhuru
wa vyombo vya habari ukiachwa na kutoingiliwa na baadhi ya viongozi wa serikali
kutasababisha wananchi kupata habari kwa kiwango cha juu na kuzidi kuiinua
tasnia ya habari nchini
Akizungumza
hii leo kwenye mdahalo wa maadhimisho ya miaka 50 ya idhaa ya Kiswahili ya
Deutsche Welle katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam,
mwanahabari mkongwe hapa nchini Jenerali Ulimwengu amesema uhuru wa vyombo vya
habari maana yake ni wahariri wa vyombo vya habari kuandika na kutoa habari
wenye uhakika nazo na kwa usahihi huku wakifuata maadili ya taaluma hiyo
Amesema
hivi sasa kumekuwa na kasumba ya baadhi ya vyombo vya habari kutokuwa na
ubunifu hasa wa kuandika vichwa vya habari vya kumvutia msomaji huku akitolea
mfano magazeti kwa kusema magazeti matano hapa nchini yanaweza kuandika kichwa
cha habari kinachofanana
“Mi
nashangaa waandishi wa habari wa siku hizi unakuta magazeti matano yanavichwa
vya habari vinavyofanana, Tundu Lissu awasha moto bungeni, CHADEMA wawasha moto
Mwanza, mara Bunge lawaka moto, sasa unajiuliza kama kila mahali moto unawake,
siku hitilafu hata ya umeme ikatokea bungeni na kuunguza jingo la bunge hivi
wataandika nini?” alisema Ulimwengu
Amesema
ni vyema waandishi wa habari pia wakajijengea desturi ya kusoma vitabu angalau
ndani ya miezi mitatu uwe umesoma kitabu, na mwandishi wa habari ambaye hawezi
ni vyema akaachana na taaluma hiyo na kwenda kufanya mambo mengine
Kwa
upande wake Mohamed Abdulrahaman kutoka DW amesema kwa kiasi kikubwa kituo
hicho kimepiga hatua na kinajivunia vipindi mbalimbali ikiwemo mbiu ya mnyonge
ambayo imekuwa ikiibua sauti za watu ambao ni nadra kuzisikia kutokana na
unyonge wa watu hao, huku akiwasisitiza waandishi wa habari kuwa na uwelewa wa
kutosha kuliko watu wengine ili kuwa na uhakika wakati unatangaza ama unatoa
habari yako
Mmoja
ya washiriki wa mdahalo huo kutoka Chuo cha uandishi wa habari cha DSJ
aliyejitambulisha kwa jina la Samia amesema katika madhimisho ya miaka 50 ya DW
bado habari za vijijini zimekuwa hazisikiki hivyo ni vyema waandishi wa habari
wakajikita vijijini kuchukua habari kwa kuwa zipo nyingi
“Waandishi
wengi wanakaa mijini wanag’anga’nia Dar es Salaam sasa hbari za vijijini
ziandikwe na nani, nendeni vijijini, nendeni kule Chamwino ndani ndani mtuletee
habari ndizo watu wanataka kuzisikia” alisema Samia