Vyombo vya habari vya uma hapa nchini, vimetakiwa kuachwa
vifanye kazi yake vyenyewe bila kuingiliwa na mtu yoyote kwa kuwa vina haki ya
kutoingiliwa katika utendaji wake wa kazi
Wakizungumza na mtandao huu katika maadhimisho ya siku ya
redio duniani wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wakazi hao wamesema vyombo vingi
vya uma hapa nchini vimekuwa vikiingiliwa katika utendaji kazi hali
inayosababisha uonevu kwa wengine
Kwa upande wake mwandishi mkongwe wa habari hapa nchini
Ndimara Tegambagwe amesema vyombo hivyo havitakiwi kuingiliwa na serikali,
waziri, mbunge, ama kiongozi yeyote kwani kunasababisha habari za watu wengine
kutosikika
“Wakati wa uchaguzi vyombo hivyo mara nyingi unaona
vinapendelea serikali sasa hili si nzuru, kwani vinaendeshwa kwa kodi ambazo tunalipa
watanzania wote hata wale ambao habari zao hazitangazwi kwenye vyombo hivyo”alisema
Tegambagwe
Naye Pili Mtambalike kutoka (MCT) amesema vyombo vya habari
vya uma ni mali
ya uma hivyo vinatakiwa kutangaza habari zote bila kukatazwa na mtu yoyote
tofauti na sasa ambapo inaonekana vingi vinapendelea serikali
“Hakuna haja ya kupendelea vyombo hivi vinatakiwa kutangaza
habari zote kwa usawa na si kupendelea zaidi za mwajiri ambaye ni serikali sasa
hapa uhuru haupo” alisema Bi. Mtambalike
Leo ni maadhimisho ya siku ya redio duniani ambapo mataifa
yote duniani yanaadhimisha siku hiyo
