Stori: Imelda Mtema wa GPL
Wakati watu wakisubiri kwa shauku kubwa kuona ndoa ya staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford na mchumba’ke wa kitambo ajulikanaye kwa jina moja la Dickson, mwigizaji huyo ameibuka na kauli nzito kuwa kwa sasa hataki ndoa hadi ajifungue tena.

Akizungumza na mwandishi wetu, Shamsa alisema kuwa huko nyuma kabla ya kuzaa alikuwa anataka kufunga ndoa kwanza lakini akaghairi na kuamua kujifungua lakini anasema kwamba ameona mtoto ni raha zaidi hivyo anataka kuongeza mwingine kisha ndiyo ndoa ifuate.
“Kwa kweli nimeona raha ya mtoto ‘so’ nimeamua kuahirisha ndoa yangu kwa sasa hadi nitakapopata mtoto wa pili,” alisema Shamsa.
Staa huyo aliongeza kuwa kufanya hivyo siyo kwamba anamrusha danadana mchumba’ke bali ameona nafsi yake itakuwa na amani na upendo utazidi maradufu kwani anapenda sana watoto.
“Si kwamba simpendi mchumba wangu, tunapendana na tunapenda sana watoto, suala ya ndoa litakuja ngoja tuzae kwanza,” alisema Shamsa.