INASIKITISHA:KAHABA AJIFUNGUA, AUA KICHANGA



Afisa polisi akikiokota kichanga hicho kilicho tupwa na kahaba

Stori:Dustani Shekidele, Morogoro wa global publishers
MTOTO mchanga hivi karibuni ametupwa katika Mto Kikundi mjini hapa akiwa amekufa, jirani kabisa na kambi ya makahaba wanaofanya biashara ya kuuza miili yao ‘machangudoa’. Baadhi ya watu walioshuhudia mwili wa kichanga hicho walimwambia mwandishi wetu kuwa kichanga hicho kilitupwa na mmoja wa makahaba, hali iliyozua tafrani kwani wasichana wanaoaminika kuwa ni makahaba walikuwa wakiipinga kauli hiyo.

“We mpigapicha usiamini hayo wanayosema hao watu... tuna ujinga kiasi gani tuzae, tuue kisha tutupe mtoto sehemu yetu ya kazi?” alihoji msichana mmoja ambaye alikataa kujitambulisha.

Hata hivyo, wasichana waliojitambulisha kwa majina Pendo Komba, Rose Joseph na Amanda Athuman kwa nyakati tofauti walisema wanaofanya unyama huo ni makahaba japokuwa wenyewe wanakataa.

Walidai kuwa hii ni mara ya sita kwa watoto wachanga kutupwa kwenye eneo hilo.

Afisa mmoja wa polisi aliyekuwepo eneo hilo, (jina tunalihifadhi) wakati wanauchukua mwili wa kichanga hicho alisema wanamtafuta mwanamke aliyefanya ukatili huo ili afikishwe mahakamani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo