RAIS KIKWETE AITEMBELEA FAMILIA ILIYOFIWA NA WATU 8 KWA AJALI


Hii ndio ajali iliyosababisha vifo vya familia hizo. Na picha za juu ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kufuatia ajali ya barabarani maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na lori. (Picha na Ikulu)

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete Februari 16, 2015 amekwenda kuhani na kufariji ndugu, jamaa na 
marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kufuatia ajali ya barabarani maeneo 
ya Kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi mkoani Pwani iliyotokea Februari 11, 2013 na kupoteza
 hapohapo maisha ya watu tisa wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze-
baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso 
kwa uso na roli la mizigo.

Familia alizokwenda kuhani na kuzifariji ni pamoja na za marehemu Hassan Erasto Kurunge (57), 
Maria Sadiki (52) na mtoto wa mwaka mmoja Samweli Ismail wa kata ya Ubena. Wengie ni 
marehemu Essau Enos Mwamgingo (16), Stella Isaack Kazimoto (18), Bahati George Mbena (17) 
na Latifa Maneno (17) 

Akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza na Mkuu wa Wilaya 
ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, Rais Kikwete alieleza kusikitishwa kwake kwa ajali hiyo, na 
kuwataka madereva wawe makini katika kuzingatia sheria za usalama barabarani

Rais Kikwete alisikitishwa zaidi kwa taarifa kwamba gari hilo dogo lilikuwa limebeba abiria 
wanane, na kuwa dereva wake ambaye pia alipoteza maisha, hakuwa makini katika kuzingatia
 sheria za usalama barabarani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo