Rais Jakaya Kikwete Amteua Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR) kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam.

  Balozi Mwanaidi Sinare Maajar
--
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR) kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam.

Aidha,kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamillius Membe (Mb.) amewateua Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa ni:-
1. Bw. Dushhood M. K. Mndeme
2. Mhe. Balozi Abdi Mshangama
3. Mhe. Dkt. Leonidas Mushokolwa
4. Mhe. Dkt. Harold Utouh
5. Mhe. Saidi Mtanda (Mb.)
6. Mhe. Betty Machangu (Mb.)
7. Bw. Affan Othman Maalim
8. Bw. Abdurahaman Abdallah
 
Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe hao ni kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 22 Januari, 2013 hadi tarehe 21 Januari, 2016.


IMETOLEWA NA: 
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM 15 FEBRUARI, 2013


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo