
Monika Akipekua Nyarayi akajifungua mtoto wa tatu Yeremiea baada ya kutelekezwa akiwa na Miimba ya Miezi 5
Monika
Isaya (25) Aliyetelekezwa na watoto watatu na Mumewe Mkuyu Juma
aliyekuwa akifanya kazi Basi la Bin Salum, wakizurula mitaani
Na Bryceson Mathias, Morogoro
MKAZI wa
Hembeti Mvomero Monica Isaya (25) aliyetelekezwa na Mumewe Mkuyu Juma
akiwa na Mimba ya Miezi Mitano ya Mtoto wa Tatu amesema, amechoshwa
kulea watoto wake watatu waliozaa na mumewe kutokana na kushindwa
kujikimu hivyo ameamua anywe sumu ili afe apate kupumzika.
Isaya alisema
hayo alipohojiwa na Mwandishi hivi karibuni akiwa analia wakati akipita
mitaani kutafuta Riziki, huku akiwaongoza watoto wake wawili
wanaotembea, Tatu Mkuyu (8), Ayubu Mkuyu (4) na Yeremeia Mkuyu (Miezi
Miwlii) aliyebebwa mgongoni.
Akielezea kisa
cha kutelekezwa Isaya alisema, “Nilikwenda kwenye Msiba wa Bibi Mzaa
Baba Hembeti MVomero, niliporudi nyumbani nilikamata Mume wangu Ugoni
akiwa na Mke mwingine nyumbani mwetu, ambapo kesho yake alitoroka na
mwanamke huyo na kwenda naye Dar es salaam na kunitelekeza na watoto
wawili huku akiniacha na Mimba ya Miezi mitano”.alisema Isaya
Alisema Mumwe
anaitwa. Mkuyu Ayubu Mweyeji wa Singida Kijiji cha Mnene ambaye alikuwa
anafanya kazi kwenye Basi la Abiria la Bin Salim linalofanya safari zake
kati ya Dodoma na Dar es Salaam, na pia alidai tangu aondoke 8.12.2012
hajui Nguo za Watoto, Malazi, Chakula ila yeye ndiye aayehangaika hivyo
kwa hivi sasa amechoka, uamuzi alionao anaona heri anywe sumu afe
kuliko kupata mateso.
Aliongeza
kwamba, Nyumba waliyokuwa wamepanga na mumeo baada ya kuwatelekeza
walishndwa kulipa Kodi kwa mwenye nyumba, naye akachukua Jukumu la
kuwafukuza na sasa amehifadhiwa na Mama mmoja ambaye ameamua kumsaidia
Bure yeye na watoto.
Mwanamke huyo
amekuwa akiwatunza watoto hao kwa kufanya vibarua vya kumwaga Nzege ili
awavishe, awalisha na kuwapa mahali pa kulala malaika wa Mungu hao,
jambo ambalo limemfanya afa yake kuwa nyong’enyevu kutokana na kazi
ngumu zinazomzidi uwezo.
Aidha Isaya
ambaye alisoma Shule Sekondari Chamwino Ikulu 2002-2004 na kuishia
Kidato cha Tatu baada ya kuugua na kushindwa kurejea Shuleni, baadaye
hali yake iliimarika wenzake wakiwa wameshamaliza masomo, hivyo
kufanikiwa kuolewa na Mkuyu ambaye amemtelekeza, huku akimtaja Baba yake
kuwa ni Husulu Isaya na Marehemu mama yake ni Mahawi Shilonyana.
Hata hivyo
alipoulizwa kama ana mawasiliano na mumewe alisema hana ila alimuachia
simu Na. 0766-430026 akidai atakuwa anampigia, lakini alipiga siku mmoja
akmtaka aongee na mke mwenzie jambo alilopata hasira akafuta Namba
yake. Pia alisema amekwenda Ustawi wa Jmii hadi Polisi ili wamsaidie
kutunza watoto au kumkamata wanasema wameshindwa kumpata na ustawi
wanadai hawana la kumsaidia.
