Mkuu wa mkoa wa
Pwani Mwantumu Bakari Mahiza ameamuru viongozi wa kata na vijiji kulinda alama
za barabarani ambazo huaribiwa kwa makusudi na nyingine kuibiwa hali
inayochangia ongezeko la ajali za barabarani mkoani humo
Mkuu huyo wa mkoa
amesema hayo katika kikao na TANROADS mkoa wa Pwani na kusema uharibifu huo
unaofanywa kwa alama za barabarani hasa kwenye maeneo yanayoongozwa na viongozi
hao wa vijiji na kata na wao kukaa kimya ni kutoitendea haki serikali