MH. LOWASSA AZUNGUMZIA VURUGU ZA BUSERERE,MKOANI GEITA


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa,
amewataka vingozi wa dini nchini, kusaidia na kurejesha hali ya amani
kati ya wasilam na wakiristo ambayo inaonekana inaanza kupotea.

Akizungumza hayo nyumbani kwake Monduli, wakati alipokuwa akipokea ujumbe kutoka kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Lowassa amesema vurugu na mauaji yaliyotokea huko Buserere, yanasikitisha sana na kuongeza kuwa ni dalili mbaya ya kutoweka kwa amani ya Tanzania.

``Rais ameelezea masikitiko yake, kwa kweli inasikitisha sana, mimi nawaomba
viongozi wa dini na madhehubu yote wasimamie na kuzuia mambo haya,
nawaomba watanzania wenzangu tusali kwa imani zetu kuomba amani yetu
isipotee`` alisema Lowassa kwa masikitikiko makubwa.

Katika fujo hizo za Buserere,mchungaji mmoja wa kanisa la sabato aliuwawa
baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya waislam na wakristo.Chanzo cha
mapigano hayo kilikuwa ni wakristo kuamua kuchinja ng'ombe na kuuza
kwenye bucha lao, hatua iliyopingwa na wananchi wa dini ya kiislam
kwenye eneo hilo.

Ujumbe huo uliyofika nyumbani kwa Mh Lowassa ukiongozwa na msaidizi wa askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya kusini mashariki mwa ziwa victoria, ulifika
kumshukuru kutokana na kusimamia na kuendesha harambee ya ujenzi wa
kanisa kuu la Shinyanga January mwaka jana ambapo zaidi ya shillingi
millioni 200 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo