Gazeti la Daily Post liliripoti
leo asubuhi kwamba msanii Goldie ambae aliiwakilisha Nigeria kwenye
jumba la Big Brother 2012 anazikwa leo, baada ya muda kupita ndio
nimezipata hizi picha za msiba wa Goldie ambae alifariki siku ya
Valentine feb 14 2013.
Imeripotiwa kwamba manenoya
mwisho ya Goldie yalikua ni kumuomba baba yake amuombee apone maumivu
makali ya kichwa aliyokua nayo ambapo Daily Post wameripoti tena kwamba
staa huyo alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali, foleni ya magari
siku hiyo ya wapendanao ilichangia kuchelewa kufika hospitali.
Chanzo mojawapo cha kifo chake ni shinikizo la damu na maradhi ya moyo.
credits:millardayo.com