Na Ibrahim Yassin,Mbeya
KAMATI ya madiwani wa chama cha demokrasia na maendeleo
(CHADEMA)wameitaka halmashauri ya wilaya ya Kyela kuwapa ufafanuzi juu ya
kudhorota kwa mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi zilizojengwa katika kijiji
cha ibanda kata ya busale wilayani hapa wakati fedha za ujenzi huo zilikwisha
tengwa,
Akitoa kauli hiyo jana
kwenye kikao cha pili cha baraza la madiwani msemaji wa kambi ya
upinzani Msyani msyani alisema kuwa halmashauri ya wilaya ya Kyela ilitenga fedha Tsh
mil 70 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi lakini nyumba hizo
zimetelekwezwa bila kukaliwa na watumishi hao,
Alisema kuwa anashangazwa na kitendo cha mwenyekiti wa
halmashauri hiyo kulifumbia macho swala hilo wakati kodi ya wananchi imetumika kujenga majengo
hayo na badara yake anabariki kutolewa fedha nyingine million 7,kukarabati jengo la zamani kwa ajili ya kuishi
mkurugenzi wa halmashauri wakati majengo
mapya ya watumishi yamejengwa na watumishi hao wamegoma kuishi katika nyumba hizo kwa madai
kuwa hazina hadhi na zipo nje ya mji,
Aidha msemaji huyo wa chadema pia aliomba ufafanuzi mwingine
wa kuhusu makusanyo ya ushuru wa ujenzi
kwenye vibali ,tenda za ujenzi ,ushuru wa mali,ushuru wa mbao,mafuta ya
mawese,mbosa,korosho,kakao pamoja na kodi za nyumba za halmashauri kuwa fedha iliyotajwa ni ndogo ukilinganisha na fedha zilizo
kusanywa,
Pia alihoji kipengele cha utawala ngazi ya kata ambayo
makisio yake yalikuwa ni million 20,kwa kata zote kwa maana kila kata inatakiwa
ipewe Tsh milioni 1,lakini wamekuwa wakipata Tsh 750.000 tu,na wanataka kujua
fedha nyingine zinako kwenda wakati shughuri za maendeleo ya kata zinazidi
kudorora,
Kamati hiyo ya
chadema walitaka kupewa ufafanuzi pia juu ya
ukarabati wa jokofu la kuhifadhia maiti
katika hospitali ya wilaya ambapo wao kama chadema hawaridhishwi na mpango huo
wa kutengeneza kwa sababu kila wanapotengeneza linaharibika,na kuitaka
halmashauri hiyo kununua jokofu jigine ili kufanikisha huduma bora katika
kitengo cha mochwari,
Akitoa majibu hayo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Gabriel Kipija alisema kuwa tatizo la kutohamia watumishi kwenye majengo
ya ibanda ni kwa sababu kuna baadhi ya sehemu katika majengo hayo yanahitaji
ukarabati ikiwa ni pamoja na umeme,na
kwamba inahitajika Tsh million 45 ili kukamilisha ujenzi huo na watumishi
watahamia pindi ujenzi huo utakapo kamilika,
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Kyela,Abdalah
Mfaume kwa upande wake alisema kuwa ni kweli mapungufu yaliyotolewa na
kambi ya upinzani yapo na kudai kuwa tatizo lililopo ni kwamba fedha za ruzuku
kutoka Serikali kuu hazifiki kwa wakati,hivyo katika bajeti hii ya mwaka wa
fedha 2013-2014,zitakapo kuja kwa wakati watakamilisha mahitaji yote