BWAWA LA MTERA LAPATA HASARA YA BILIONI 740


Na Oliver Motto

SHIRIKA la Umeme Tanzania- TANESCO limepoteza mapato ya shilingi Bilioni 740    kutokana na maji katika Bwawa la Mtera kukauka, huku likiingia hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni 403 kwa kutumia nishati  ya mafuta ili kuendesha mitambo yake.

Hayo yalizungumzwa na meneja mkuu wa Tanesco Mtera, Injinia Nazir Kachwamba, wakati wadau wa mikoa na Wilaya zinazopitiwa na bonde la Rufiji walipotembelea mgodi huo wa uzalishaji wa nishati ya umeme, kwa lengo la kutambua changamoto zinazolikabiri Bwawa la Mtera, kutokana na vyanzo vya maji kuharibiwa, na hivyo mto mkuu ruaha kushindwa kutiririsha maji na kusababisha Bwawa hilo  kukauka.

Nazir alisema kupungua kwa maji kwa kiwango kikubwa katika Bwawa hilo, kunasababisha grid hiyo kutumia nishati nyingine za kuendeshea mitambo, na hivyo kuingia gharama kubwa tofauti na kiwango halisi cha uzalishaji na hivyo kupata hasara.

“Vile vile kutokuwepo kwa Hydro ya kutosha kunaathiri uzarishaji wa grid, kwani mitambo ya maji inafua umeme kwa haraka bila kuathiri uzalishaji, tofauti na nishati nyingine za mafuta, huku upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya kawaida hapa ukiwa  chini,” Alisema Injinia Nazir.

Aidha alisema kutokuwepo kwa maji katika Bwawa hilo la Mtera kumesababisha uzalishaji wa umeme kutokuwa wa kutosha na hivyo kuyumbayumba juu ya uendeshaji wa mitambo, licha ya kuwa .

Alisema hali hiyo inatokana na wananchi kufanya uchepushaji wa maji mengi pasipo kuwa na vibali, kwa shughuli mbalimbali za kibinadamu kama kilimo na hivyo kusababisha hasara kubwa kwa mgodi huo.

Alisema kwa kawaida mitambo hiyo inaweza kuvumilia kutembea hadi mita 687.00 mita mbili kwenda chini na sasa wapo mita 688.84, kiwango cha juu cha matumizi, ambapo walilazimika kuomba kibari wizara ya maji ili kuendelea kutumia maji hayo na kupata ruhusa ya kutumia mita mbili na nusu nyingine kwenda chini.

Alisema kupungua kwa maji kwenye Bwawa athari zake ni nyingi ikiwemo la kutumia gharama kubwa za fedha, katika kusafisha maji hayo ambayo sasa ni machafu kutokana na kutumia maji yaliyochini ya kina sahii kinachotakiwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo