Watu 35 wamefariki katika ajali ya basi karibu na mji wa Mwingi
Mashariki mwa Kenya. Jeshi la polisi limesema kuwa wengi wa waliofariki
walikuwa wanafanya kazi mjini Nairobi, na walikuwa wanarejea makwao
kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika siku ya Jumatatu.
Farah
Aden Ali, aliyenusurika kifo alisema kuwa basi hilo lilikuwa limejaa
watu kupindukia na lilianguka baada ya dereva kupoteza mwelekeo.
Barabara nyingi nchini Kenya ziko katika hali mbaya na vile vile hali ya mabasi mengi ni mbaya.
Afisa
wa trafiki Samuel Kimaru alisema kuwa takriban abiria 35 walifariki na
wengine 50 kujeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo.
Bwana
Aden Ali aliambia BBC kuwa vikundi vya uokozi viliwasili katika eneo la
ajali masaa manne baada ya ajali kutokea hali iliyosababisha waliokuwa
wamekwama ndani ya basi hilo kufariki.
Basi lilikuwa limejaa watu na lilikuwa linaelekea katika miji ya Mandera na Garisa
Ali
alisema kuwa dereva alikuwa na matatatizo na gia ya basi hilo tangu
kundoka Nairobi.
Alisema alikuwa amelala lakini aliamka muda mfupi baada
ya ajali kutokea.
“Dereva alipoteza mwelekeo. Alikua anajaribu kulirejesha basi barabarani , lakini likaanguka kwa upande,” alisema Ali.
Babaraba
za Kenya huwa na msongamano mkubwa wa magari hususan kabla ya uchaguzi
mkuu huku wafanyakazi wa miji wakielekea mashinani kupiga kura.
Source: BBC SWAHILI
Source: BBC SWAHILI