Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii aliyeko Mikumi Morogoro.
ZAIDI ya wanyama 200 wa aina tofauti 12, katika hifadhi ya Taifa ya
Mikumi,kila mwaka hufa kwa kugongwa na magari katika barabara kuu ya
Dar es Salaam hadi Zambia inayopita katikati ya hifadhi hiyo kwa
kipande cha kilometa 50.
Na kutokana na magari kupita hifadhini bila kulipia na kusababisha mauaji
ya wanyama, serikali imekuwa ikipoteza mapato ya zaidi ya Sh billion 6
kwa mwaka, Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Damiani Saru amesema.
Akiongea na waandishi wa habari 10 wa mkoa wa Kilimanjaro,
walio kwenye ziara za kutembelea hifadhi za taifa Bw Saru alisema kipande cha barabara kinachopita kwenye hifadhi hiyo kina
urefu wa kilomita 50, ambapo kuna mabango mbalimbali yakiwataka
madereva kwenda kwa mwendo mdogo lakini bado wameendelea kuendesha kwa
mwendo wa kasi unaoathiri wanyama hao.
Alisema kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita wanyama zaidi ya
wanyama 40 walikufa na baadhi ya magari yalikamatwa na kutozwa faini
kulingana na aina ya mnyama.
“Faini inayotozwa si suluisho kwani si mara zote wanagogwa wakati
askari wa wanyamapori wakiwepo mara nyingine inatokea wakati hawapo na
wahusika kukimbia na kubaki kuokota mizoga…tumefanya utafiki kwa mwaka
tungekusanya Sh billion 6 iwapo magari yote yanayopita yangelipa”
alisema.
Aliainisha wanyama wanaogongwa mara kwa mara kuwa ni swala pala ambao
huruka kwa wastani wa 15 hadi 20, samba, chui, twiga, tembo, nyani,
nguruwe na digidigi na zaidi hutokea nyakati za usiku.
Bw Saru aliongeza kuwa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa),
limewasilisha andiko kwa serikali kuelea umuhimu wa kuondolewa kwa
barabara hiyo na inavyoendelea kuwepo ina athari gani kwa mustakabali
wa wanyama na wanaednelea kusubiri majibu.
Mhifadhi huyo alisema awali waliweka kizuia kwa magari mwanzo na
mwisho wa hifadhi na kila gari kutakiwa kulipia, ili kuepusha utalii
wa bure, ujangili na kugonga wanyama, lakini Walaka wa Barabara nchini
(Tanroads) walipinga suala hilo kwa kuna barabara ni mali yao.
“Ifike mahali tiuone wanyama wanakwishwa, kulea mnyama mmoja hadi
akifie umri flani inacchukua muda mrefu, wakiendelea kuteketezwa kwa
kugongwa na ujagili hifadhini ni wazi kuwa watakwisha” alisema Saru.
Naye, Mhifadhi Utalii, Tutindaga Mdoe, alisema uwepo wa barabara hiyo
umeruhusu utalii wa bure, ambapo wageni ambao walitaka kutembelea
hifadhi huacha kwa kuwa wanaweza kupita barabarani na kupiga picha.
Hata hivyo, alisema hifadhi imechukua hatua na kuwakamata wanaofanya
hivyo, lakini kwa wanaosafiri kwa mabasi wamekuwa wakijionea wanyama
bure jambo ambalo linapunguza idadi ya watalii wa nje na ndani.