Na Ibrahim Yassin Rungwe,
ZAIDI ya wanafunzi 600 wa shule ya msingi Kisegese
wilayani Rungwe mkoani
Mbeya wapo hatarini kupata magonjwa
ya milipuko kutoakana na
kukosa huduma ya
vyoo ali inayowalazimu
wanafunzi hao kujisaidia
katika vichaka vilivyopo
pembezoni mwa shule hiyo,
Ali hiyo iligunguliwa
siku za hivi
jana na mwandishi wa gazeti hili
alipofanya ziara ya
kushtukiza katika harmashauri
mpya ya busokelo
ambapo wananchi wa
kata ya kisegese walitoa kero hizo
kuwa shule yao
imetelekezwa na serikali,
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti wananchi hao walidai kuwa
shule yao mbali na
wao kuchangia nguvu kazi katika ujenzi
wa kuiendeleza shule
hiyo lakini Halmashauri
kupitia idara ya elimu
wameshindwa wameshindwa kuchangia
nguvu kazi hizo na kuona
kuwa serikali imewatenga,
Wanannchi hao wakiongozwa
na John Mwaisumo walizitaja
changamoto zinazoikabili
shule hiyo kuwa
ni ukosefu wa matundu ya vyoo,ofisi ya
waalimu na vifaa vya ofisi, vyumba vya madarasa,madawati na
upungufu wa waalimu inayopelekea wanafunzi kushuka
kitaaluma,
Mkuu wa shule hiyo Mwl
Patric Nyimbo alikiri kuwepo na changamoto hizo katika
shule yake na kudai
kuwa,ni kwali shule hiyo ina kabiliwa
na changamoto hizo kwa muda mrefu,shule hiyo
inahitaji kupatiwa waalimu haraka
kwani waalimu waliopo ni wanne tu ukilinganisha na idadi
kubwa ya wanafunzi ambao wamezidi
600,
Mwl Nyimbo alitaja
mahitaji mengine kuwa
ni matundu 10 ya
vyoo yaliyopo ni manne,ofisi ya waalimu,meza na kabati,ambapo
kwasasa ofisi ya waalimu
wa shule hiyo imejengwa kwa
mianzi na kukosa thamani
za ndani,
Mwenyekiti wa
kijiji cha Kisegese Nasubile Mwasiku naye kwa upande
wake aliishutumu halmashauri
ya wilaya hiyo kuwa
imeshindwa kuunga mkono jitihada za wananchi
kuchangia maendeleo ya shule hiyo,na kuwa wananchi walijenga jingo la
madarasa mawili kwa mtambao
wa panya ambalo limekaa zaidi ya
miaka nane halmashauri imeshindwa kulipaua kitu ambacho kinawakatisha tama
wananchi kuchangia maemdeleo,
Diwani wa kata
hiyo Edson Mbila alikiri
kuwepo na changamoto
hizo na kudai
kuwa tayari amezipeleka kwa
afisa elimu msingi wa
wilaya ambaye waliongozana kwenda
kupeleka tatizo hilo kwa
mkurugenzi na kinacho subiriwa
sasa ni utekelezaji wa kuondoa
tatizo hilo,
Mkurugenzi wa halmashauri
mpya ya Busokelo
wilayani hapa Imelda Isuza, alikiri kupokea
tatizo hilo na kwamba tayari wametega
fedha mil 10 katika bajeti
ya mwaka 2012-2013 kwa lengo
la kuondoa changamoto hizo,ambalo
linawakatisha tama wananchi kuchangia
nguvu kazi katika kujiletea
maendeleo ya kata
hiyo.