Waziri wa Nishati na
Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo
---
Waziri wa Nishati na
Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akizungumza katika kipindi cha
Nipashe cha Radio One Stereo, amesema anawaeleza Watanzania kuwa,
uchumi wa Dunia wa sasa ni wa ushindaji, hivyo “sisi” Watanzania
tumetaka tuifanye Bandari ya Mtwara kituo kikuu cha utafiti na
uendeshaji wa shughuli zote za gesi. Kwa hivyo, Wawekezaji waliotaka
kuwekeza wakiondoka, bandari ya Mtwara kutokana na sababu zozote za
kushindwa utulivu wa kufanya kazi zao, watahamishia shughuli zao bandari
za Beira au Mombasa.
Mwandishi: Tatizo la wakazi wa Mtwara ni lipi?
Waziri: Mimi sielewi, inabidi wao waulizwe. Watu wa Mtwara kitu walicho nacho haki ni Korosho... Hizo korosho ni mali zao kabisa, mbona hizo korosho zinasafirishwa? Watanzania tuwaulize kwa nini korosho zao zinasafirishwa kutoka Mtwara.
Mwandishi: Huoni vyema nyie Serikali mkakaa na wananchi kutoa elimu kuhusiana na suala la gesi?
Waziri: Serikali na TPDC tumefanya vikao vingi sana na viongozi wa Mtwara na Lindi... wakiwemo Wabunge wao hadi

wale
wa Halmashauri wamepelekwa nje ya nchi kujifunza umuhimu unaotokana na
hiyo gesi asilia. Isitoshe, wananchi wa Lindi na Mtwara wamepunguziwa
bei ya umeme... Je, wanavyounganishiwa huo umeme kwa bei nafuu kuliko
wananchi wengine, hawajiulizi? Pili, vijana wao tumewachukua wanakwenda
kusoma VETA...
Mwandishi: Upi ni wito wako kuhusiana na vurugu, migororo?
Waziri: Kwanza naomba kuwaambia wananchi wa Mtwara, kuwa wasicheze ngoma wasiyoijua. Wasiimbe nyimbo wasizozijua wala hawajui wanaotunga tenzi za nyimbo hizo. Pili, Watanzania wote kwa miaka mingi tumepata matatizo ya umeme, suluhisho la umeme linapatikana sasa.