Na Nickson Mahundi
KAMPUNI
ya Tanzania
China Internation Minerals Resouces Limited (TCIM) inayochimba madini ya
makaa
ya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga Ludewa imeanza ukarabati wa
shule ya
msingi katika kijiji cha Mkomang’ombe wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe
baada ya
wananchi kushindwa wa kijiji hicho kushindwa gharama.
Shule
ya msingi
Mkomang’ombe iliezuliwa paa lake na vyumba vitatu kuharibiwa vibaya
kutokana na
upepo mkali kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani Ludewa
na
kusababisha uharibifu mkubwa ambao kwa mujibu wa uongozi wa kijiji
wananchi
walishindwa kumudu gharama za ukarabati.
Akikabidhi
mabati na
misumari na vifaa vya ujenzi kwa wananchi wa kijiji cha mkomang’ombe
meneja
mkuu wa uzalishaji wa makaa ya mawe na umeme Achen qi Hong alisema kuwa
kampuni
yake imeaua kutoa vifaa vya kiwandani kama mchango wa ukarabati wa shule
hiyo
baada ya kuona watoto wanakosa mahali pa kusomea.
’’’’
Tanzania na China
mbali ya ubia uliopo katika miaradi ya Liganga na mchuchuma tuna udugu
wa muda
mrefu kwa hiyo watoto wa kijiji cha cha mkomang’ombe wanapokosa masomo
tunaathirika sote kwa sababu ni watoto wetu sote.’’’’ Alisema Achen Hong
ZHAO
DAO QUAN
mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Tanzania China
International
Menerals Limited na HUANG DA XIONG ambaye ni afisa mtendaji mkuu wa
kampuni
hiyo wakaliambia gazeti hili kuwa walipokea barua kutoka kwa wananchi wa
kijiji
cha Mkomang’ombe wakiomba mchango wa vifaa vya madukani sisi hatukua na
pingamizi kwani ni sehemu ya mahusiano yetu na wananchi.
‘’’’’
huo ni mwanzo tu
si kama wawekezaji tutaendelea kushirikiana na wananchi na jamii kwa
ujumla
katika masuala yote ya maendeleo yakiwemo elimu, Afya na maji kwa kuwa
ni
mahitaji muhimu ya binadamu.’’’ Alisema Zhao mwenyekiti wa bodi ya
wakurugenzi
Mwalimu
mkuu wa shule
ya msingi mkomang’ombe John Haule akitoa taarifa kwa wafadhiri hao
alisema
shule hiyo imejengwa mwaka 1975 kwa ramani za wakati huo lakini shule
hiyo
imekuwa ikiezuliwa na upepo kila mwaka jambo ambalo kila likiezuliwa
inakuwa
mzigo wa wazazi ambao hushindwa kumudu gharama kutokana na kukabiliwa na
umaskini wa kipato.
Haule
akaongeza kuwa
kijiji kilipitisha mchango wa shilingi mia tano (500) kwa kila mwananchi
lakini
fedha iliyochangwa haikutosha kununua hata kilo moja ya misumali ndipo
tukaomba
msaada kwa wenzetu wachina ambao hawakusita kutoa mchango huo.
‘’’’’
Taarifa ya
kuezuliwa kwa shule hiyo kila mwaka tulishapeleka kwa kwa mkurugenzi wa
Halmashauri
ya wilaya ya Ludewa lakini bado haijapatiwa ufumbuzi kwa hiyo
tunaendelea
kusuasua na ukarabati kila linapotokea tatizo kwa sababu uwezo wa
kuivunja na
kujenga upya hatuna.’’’’alisema Haule
Haule
akaongeza kuwa
wanalazimika kuweka zamu ya kuingia madarasani kwa wanafunzi hasa kwa
darasa la
sita, darasa la tano, na darasa la tatu na pili kutokana na uhaba wa
madarasa
kufuatia kuezuliwa kwa madarasa hayo.
Akitoa
shukrani kwa
kampuni hiyo Diwani wa kata ya Mkomang’ombe Ananias Haule Mamba alisema
wananchi
wa kata yake wanakabiliwa na changamoto nyingi hasa katika sekta ya
elimu afya
na maji na kuongeza kuwa wawekezaji wameanza vyema hivyo ana imani
watasaidia
hata katika shughili zingine za maendeleo pale watakapotakiwa kufanya
hivyo.
Kampuni
ya Tanzania
International Minerals Limited inaendeshwa kwa ubia kati ya Tanzania na
China
katika migodi ya uchimabaji makaa ya mawe ya mchuchuma na chuma cha pua
cha
Liganga.
