VIWANGO VYA KUKODI GREDA LA MANISPAA YA IRINGA VYATAJWA


Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo  
Na  Frank Leonard ,Iringa 
HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa imependekeza viwango viwili tofauti vitakavyotumika kukodi mtambo wake wa kuchonga barabara (greda).
 
Mtambo huo ulinunuliwa hivi karibuni kwa zaidi ya Sh Milioni 581 zilizokopwa kutoka benki ya CRDB. 
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo alisema kwa wateja wa nje watakodi mtambo huo kwa Sh 800,000 kwa saa kumi.
“Na iwapo kata au mamlaka ya serikali itahitaji kulitumia gharama itakuwa Shilingi 250,00 kwa saa kumi,” alisema.
 
Pamoja na gharama hizo, Mahongo alisema wateja watalazimika pia kugharamia mafuta na dereva.
 
Aliyasema hayo kwenye kikao cha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2013/2014 na mapitio ya bajeti ya mwaka 2011/2012 na Julai hadi Desemba, 2012.
 
Akiwasilisha mapendekezo ya mapato na matumizi ya halmashauri kwa mwaka 2013/2014, Mahongo alisema wanakadiria kukusanya zaidi ya Sh Bilioni 23.3 kutokana na vianzoa mbalimbali.
 
Alisema kati ya mapato hayo zaidi ya Sh Bilioni 20.2 ni ruzuku kutoka serikali kuu na Sh Bilioni 3.1 kutoka vyanzo vya halmashauri.
Wakati huo huo, kikao hicho kilipokea maoni yaliyotolewa na kamati mbalimbali za kudumu za halmashauri hiyo.
 
Baadhi ya maoni hayo ni pamoja na kuboresha masoko ya Kihesa na Mashine Tatu ili yasadie kuongeza mapato ya halmashauri.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo