Kituo cha Utangazaji kupitia Runinga cha ITV, ambacho ni miongoni
mwa vituo mahiri Barani Afrika, kimetangazwa rasmi kuwa kituo bora
nchini kwa mwaka 2013/14, kupitia tuzo za ubora wa makampuni
‘Superbrands’ zinazoratibiwa na Kituo cha Utafiti wa Viwango vya Ubora
na Ufanisi katika Huduma za Makampuni (TCBA) kilichopo London,
Uingereza.
Tafiti zilizofanyika zimeshirikisha maoni na mitazamo kwa pande zote yaani Baraza la Wataalamu, na zaidi ya watumiaji wa huduma 600, na baadaye kutembelea Vituo vya utafiti vya kimataifa vilivyopo nchini vya TNS RMS, kwa minajiri ya kutazama na kuangalia mwenendo wa ubora na uimara wa makampuni.
Taasisi ya Superbrands, ambayo ni taasisi kubwa kuliko zote duniani inayoratibu ubora na thamani ya nembo za Superbrands, kwa makampuni yanayotoa huduma zinazokubalika na walaji, inatoa huduma zake kwa zaidi ya mataifa 90 duniani kote. TNS RMS pia inakubaliana na huduma zake.
Tuzo za Superbrands ni miongoni mwa tuzo zenye thamani kubwa na zinazoleta heshima ya pekee ndani ya Kampuni. Hii ni mara ya tatu kwa tuzo hii kutolewa ndani ya ukanda huu wa Afrika ya Mashariki.
Maamuzi na hatimaye utoaji wa tuzo husika yanatoka Baraza Huru la Wataalamu waliobobea katika masuala ya Biashara lakini lengo hasa likiwa ni kustawisha na kuhamasisha ari katika utoaji huduma zinzozingatia ubora.
Taasisi hiyo ya Superbrands, kama inavyofahamika taasisi kubwa kuliko
zote duniani inayoratibu ubora na thamani ya nemboza Superbrands, kwa
makampuni yanayotoa huduma zinazokubalika na walaji kwa malengo ya
kuboresha ubora wa huduma kwa mlaji ITV, ambayo huko nyuma haikuingizwa
katika orodha ya juu ya ubora kwa sasa imeshika kasi kubwa na kuibuka
mshindi kwa mwaka huu 2013/14 na kupelekea kukipita Kituo cha Utangazaji
cha Clouds FM ambacho kimeshika nafasi ya pili.
Nafasi ya 3 katika tafiti imeshikiliwa na maji ya kunywa ya Kilimanjaro, ikifuatiwa Chai Bora na Kampuni ya Kimataifa ya Panadol na Azam, iliyokuwa kileleni katika tuzo zilizotolewa mara ya mwisho na sasa imeshika nafasi ya 12.
Nafasi ya 3 katika tafiti imeshikiliwa na maji ya kunywa ya Kilimanjaro, ikifuatiwa Chai Bora na Kampuni ya Kimataifa ya Panadol na Azam, iliyokuwa kileleni katika tuzo zilizotolewa mara ya mwisho na sasa imeshika nafasi ya 12.