Soko
kubwa la mahindi linatarajiwa kujengwa kwenye kata ya Engusero wilayani
Kiteto ili kuwanufaisha wakulima wake na kuwawezesha wauze mazao yao
karibu
pindi wakiyavuna mashamabani.
Taarifa
hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo Martha Umbulla,wakati akiongea na
vyombo vya habari kuhusiana
na mafanikio ya Serikali ya awamu ya nne na utekelezaji wa ilani ya
CCM,mwaka
2005 hadi Desemba 2012.
Pia
alisema kuwa lengo la kujenga soko hilo kwenye kata ya Engusero ni
kuhakikisha wakulima wanainufaisha wilaya hiyo kwani hivi sasa wanauza
mazao
yao kwenye soko la Kibaigwa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.
Aliongeza
kuwa mwaka jana walifanikiwa kuzalisha zaidi ya tani 120,000 za mahindi
hivyo watatumia fursa hiyo kwa kujenga soko lao eneo la Engusero kwani
robo
tatu ya mahindi yanayouzwa kwenye soko la Kibaigwa yanatokea Kiteto.
Aidha
aliendelea kusema kuwa asilimia 80 ya wakulima wa wilaya ya Kiteto
wanajishughulisha na kilimo cha mahindi na pato la wilaya hiyo
linategemea
kuchangiwa kupitia mazao ya kilimo kwa asilimia 38 na wakulima 156,199
wamepatiwa mafunzo.
Mkuu
wa wilaya hiyo ameeleza kuwa wa upande wa kilimo cha umwagiliaji
wameandaa
skimu za umwagiliaji kwenye vijiji vya Sunya,Olgila na Ngipa ambapo
wakulima
wake wanajihusisha na kilimo cha mahindi na mbogamboga.
‘’Waandishi wa habari pamoja na
hayo tumepiga hatua kubwa kwenye
suala la kilimo kwani tumetenga kilomita za mraba 3,800 kwa ajili ya
kilimo cha
mazao mbalimbali ikiwemo mahindi,alizeti,mbaazi na mtama mweupe,”
alisema
Umbulla.
Aliongeza
kuwa kupitia vikundi vya kuweka na kukopa (Saccos),benki za jamii
vijijini (Vicoba) na vyama vya ushirika (Amcos) wana vikundi hao hutumia
hisa
zao kwa kununua mazao na kuyahifadhi ghalani na kuyauza pindi bei ya
mazao ikipanda.
Alisema
kuwa hivi sasa wakulima wengi wa wilaya ya Kiteto wamepiga hatua kubwa
katika
uhifadhi wa mazao ghalani ili waendeshe shughuli za maisha wakati wa
kusubiri
bei ya mazao ipande ndipo waweze kuiuza.