Mtangazaji wa Kitulo Fm Aldo Sanga (kulia) akimhoji mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula
Mwenyekiti wa umoja wa makanisa wilaya ya Makete Padri Haule akizungumza na mtandao huu
katibu wa CCM wilaya ya Makete Bw. Miraji Mtaturu
Mtangazaji wa Kyela Fm na mwandishi wa gazeti la majira bw. Israel Mwaisaka
Serikali imepongezwa kwa kuanzisha utaratibu wa kutoa
taarifa ya mafaniko ya serikali kwa wananchi wake kila baada ya miezi minne na
kusema kuwa utaratibu huo utasaidia wananchi kuwa na imani na serikali yao
Wakizungumza na wanahabari mara baada ya Mkuu wa wilaya ya
Makete Josephine Matiro kusoma taarifa ya mafanikio ya serikali ya awamu ya nne
tangu 2005-2012, wadau hao wamesema hali hiyo itasaidia hata wao kutoa maoni yao kuhusu serikali pale
itakapoonekana mambo hayaendi sawasawa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Bw.
Francis Chaula amesema wao kama chama
wanaupongeza utaratibu huo kwa kuwa ni mzuri na unaweka wazi shughuli
zinazofanywa na serikali na wali ilipofikia
“Unajua sasa hivi ni rahisi kuishauri serikali pale
itakapotoa taarifa na kuelewa wapi tulipotoka tulipo na tunapoelekea
Naye katibu wa CCM wilaya ya Makete amesema utaratibu huo
ulikuwa ni maazimio ya mkutano mkuu wa chama hicho wa mwaka jana, na utasaidia
kuondoa upotoshwaji unaofanywa na vyama vya kisisa kuwa serikali haifanyi kazi
Mbali na hilo amesema ukimya
wa baadhi ya watendaji wengi wa serikali ndiyo ulipelekea kutotolewa kwa
taarifa hizi na hivyo utaratibu huu utasaidia wananchi kupata taarifa za
maendeleo ya serikali yao
“Isifike sehemu uchaguzi ukaonekana ni sehemu nzuri ya
kueleza serikali imefanya nini, hiyo siyo sahihi mi nadhani jukumu kubwa kama CCm ni kuendelea kuikumbusha serikali kutekeleza
wajibu wake na tuachane na upotoshaji unaotolewa huko nje jamani tuupuuze”
alisema Mtaturu
Mwenyekiti wa makanisa wilaya ya Makete Padri Haule amesema
utaratibu huo pia utasaidia wao kama viongozi
wa dini kwenda kuwaelezea wananchi mafanikio ya serikali hivyo serikali
inatakiwa kuwapatia taarifa hizo ili wazitumie kuwaelewesha
Hata hivyo Sheikh wa wilaya ya Makete Anuari Sanga amesema
utaratibu huo kwa kuwa unashirikisha wadau mbalimbali wanaofanya kazi na
serikali ikiwemo viongozi wa dini, watapata fursa ya kuishauri na kutoa maoni yao pale wanaposomewa
taarifa hiyo